Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-AFGHANISTAN

Waziri mkuu wa Australia, Julia Gilard atangaza kuviondoa vikosi vya nchi yake nchini Afghanistan ifikapo 2013

Serikali ya Australia kupitia Waziri Mkuu wake Julia Gillard ametangaza rasmi wataondoa vikosi vyake vilivyo nchini Afghanistan kwenye Jeshi linaloshika doria chini ya mwanvuli wa NATO yataondolewa mapema zaidi tofauti na muda uliopangwa. 

Waziri mkuu wa Australia, Julia Gilard wakati akitangaza mpango wa nchi yake kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan
Waziri mkuu wa Australia, Julia Gilard wakati akitangaza mpango wa nchi yake kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Gillard amesema vikosi vyao vilivyopo nchini Afghanistan vitaoneolewa mwaka mmoja kabla, kauli inayokuja wakati huu ambapo Rais Hamid Karzai akivishutumu vikosi hivyo kushindwa kuzima mashambulizi yaliyotekelezwa na Wanamgambo wa Taliban.

Gillard amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na uwezo wa Vikosi vya Afghanistan kuweza kuchukua jukumu la kulinda amani tofauti na ambavyo imekuwa imepangwa na NATO kuacha jukumu hilo mwaka elfu mbili kumi na nne.

Australia imekuwa na vikosi vya kulinda amani nchini Afghanistan toka kuanza kwa vita nchini humo mwaka 2003 wakati ambapo majeshi ya NATO na Marekani yaliingia nchini humo kwa lengo la kuwasambaratisha wanamgambo wa Taliban.

Mataifa mengi ya Ulaya ambayo yanavikosi vya kulinda amani nchini Afghanistan vimetangaza kuondoa vikosi vyao ifikapo mwaka 2014 mwaka ambao pia majeshi ya NATO yamesema kuwa yatakuwa yameondoa vikosi vyake vyote.

Hatua ya waziri mkuu Gilard kutangaza kuviondoa vikosi vyake mwaka mmoja kabla ya mwaka wa mwisho imeelezwa kuwa ni yakisiasa zaidi huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa analenga kujijengea umaarufu kisiasa.

Kauli ya Gilard imeungwa mkono na wabunge wengine wa upinzani ambao nao wamekuwa wakishinikiza nchi hiyo kuondoa vikosi vyake nchini humo kwa kile walichoeleza kuwa nchi imekuwa ikutumia gharama kubwa kuwahudumia wanajeshi wake walioko nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.