Pata taarifa kuu
MALI

Rais wa Mpito Nchini Mali Traore aapishwa na kuahidi wapo tayari kupambana na Waasi wanaoshikilia sehemu ya Kaskazini

Kiongozi Mpya wa Mali ambaye amepishwa kuongoza serikali ya mpito Dioncounda Traore na kutoa kitisho kwa Waasi wa Tuareg na Makundi mengine ya Kiislam yanayoshikilikia eneo la Kaksazini mwa nchi hiyo wawe tayari kwa vita madhubuti. Traore ambaye ni Spika wa Bunge wa zamani anashika wadhifa huo kutoka Kiongozi wa Kijeshi Kepteni Amadou Haya Sanogo aliyeiangusha serikali ya Rais Amadou Toumani Toure baada ya kushindwa kukabiliana na Waasi wa Kaskazini.

Kiongozi Mpya wa Mali Dioncounda Traore ambaye ameapishwa kushika wadhifa huo kuongoza serikali ya mpito
Kiongozi Mpya wa Mali Dioncounda Traore ambaye ameapishwa kushika wadhifa huo kuongoza serikali ya mpito
Matangazo ya kibiashara

Rais Traore amekula kiapo chake na kuahidi kulinga Jamhuri ya Mali na kuheshimu Katiba huku hotuba yake ikiwatoa wasiwasi wananchi wa Bamako juu ya suala la usalama kwani wapo tayari kupambana Kijeshi na Waasi ambao ni tishio huko Kaskazini.

Traore amewataka Waasi kuacha mara vitendo vinavyokwenda kinyume na haki za binadamu ikiwemo ubakaji na kuondoka katika Miji yote ambayo wameiweka kwenye himaya yao kinguvu.

Kiongozi huyo ambaye anatarajiwa kukaa madarakani katika kipindi cha mpito kabla ya kuitisha uchaguzi wenye lengo la kurejesha utawala wa kiraia amesema bila ya kusita wataingia vitani kukabiliana na waasi hao.

Traore amesema suluhu pekee kwa waasi hao wa Tuareg ni kuweka chini silaha na kukubaliana na utawala wa kiraia ambao umeingia madarakani sambamba na kurudisha miji yote waliyoiteka chini ya serikali ya Bamako.

Rais Traore ameingia madarakani baada ya uwepo wa mazungumzo baina ya pande zilizokuwa zinahasimiana chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wakiongozwa na Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore.

Makubaliano baina ya Kiongozi wa Kijeshi Kepteni Sanogo na Rais Toure ndiyo ambayo yalichangia Kiongozi huyo wa nchi ajiuzulu na kupisha mchakato wa kidemokrasia kuchukua nafasi yake kurudisha utawala wa kiraia.

Kikwazo kikubwa ambacho anakabiliwa nacho Rais Traore kwa sasa ni kuhakikisha anakabiliana na Waasi wa Tuareg ambao wamejitangazia Utawala wa eneo la Azawad wakisema wamejitenga rasmi na serikali ya Bamako.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.