Pata taarifa kuu
CANADA

Canada yawa nchi ya kwanza kujitoa kwenye Utekelezaji wa Mkataba wa Kyoto

Canada imekuwa nchi ya kwanza kujiondoa rasmi kwenye utekelezaji wa Mkataba wa Kyoto wa mwaka elfu moja mia tisa na tisini na saba ukiwa na lengo la kudhibiti Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na kupunguza uwepo wa hewa ya ukaa inayochangia na kuongezeka kwa viwanda duniani.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mazingira wa Canada Peter Kent ndiyo ambaye ametangaza uamuzi wa nchi hiyo kujitoa kwenye utekelezaji huo wa Mkataba wa Kyoto akisema nchi yake haiamini kama njia hiyo ndiyo itakuwa sahihi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Waziri Kent amesema kuwa ilikuwa ni kosa kwa nchi yake kuweza kusaini mkataba huo kwa kuwa nchi kama Marekani, China na Urusi zenyewe zimekuwa hazitekelezi kile ambacho kipo kwenye makubaliano ya kudhibiti ongezeko la hewa ya ukaa duniani.

Canada imesema kutotekelezwa kwa makubaliano yaliyopo kwenye Mkataba wa Kyoto wa mwaka elfu moja na tisini na saba inadhihirisha kutokuwepo kwa umuhimu wa mkataba wenyewe na ndiyo maana wamefikia hatua kujitoa kwenye hilo.

Canada imesema kuwa haioni kama makubaliano mapya ambayo yamefikiwa na nchi zilizoshiriki kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi huko Durban nchini Afrika Kusini kama yanaweza kusaidia kule amabadiliko ya aina yoyote ya kupata suluhu ya hali hiyo.

Uamuzi wa Canada kujitoa kwenye utekelezaji wa Mabadiliko ya Tabia Nchi unakuja wakati Mkutano kama huo ukiwa umemalizika mwishoni mwa juma lililopita ambapo Mataifa ya Afrika yaliweka shinikizo la kutaka mataifa makubwa kutekeleza kwa vitendo mkataba huo wa mwaka elfu moja mia tisa tisini na saba.

Tayari nchi ya China imelaumu hatua ya Canada kujiondoa kwenye utekelezaji wa Mkataba wa Kyoto ambao ni muhimu sana kwa mustakabali wa dunia kwani unaweza ukasaidia kulinda mazingira na hata kudhibiti athari kwenye anga la ozoni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Liu Weimin amesema hatua hiyo itakwamisha juhudi za Jumuiya ya Kimataifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yamechangia hata mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa sasa.

Kuanza kujitoa kwa mataifa makubwa kwenye utekelezaji wa Mkataba wa Kyoto unaiweka rehani Afrika ambayo nchi zake zimekuwa ndiyo muathirika mkubwa wa mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea duniani kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.