Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Rais Hugo Chavez akiri kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe wa saratani mwilini

Rais wa Venezuela Hugo Chavez kwa mara ya kwanza amejitokeza kwenye Televisheni ya nchi hiyo na kumaliza minong'ong'ono iliyokuwa imetanda nchini mwake juu ya hali yake baada ya kuripotiwa yupo Cuba kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua. 

Rais wa Venezuela Hugo Chavez akihutubia kwa njia ya Telesheni kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji
Rais wa Venezuela Hugo Chavez akihutubia kwa njia ya Telesheni kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji REUTERS/VTV via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Rais Chavez amejitokeza kwenye Televisheni na kuwambia wananchi wake waliokuwa na hofu ni kweli amefanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa saratani ambao ulikuwa unamsumbua kwa muda sasa.

Kiongozi huyo wa Venezuela amesema wataalam wa masuala ya tiba waliomfanyia uchunguzi walibaini ana uvimbe huo wa saratani na ikalazimika afanyiwe upasuaji  nchini Cuba.

Rais Chavez amekiri kufanyiwa upasuaji mara mbili kwanza ilikuwa ni kuondoa huo uvimbe wa saratani na kisha Madaktari wakalazimika kumpasua tena kuondoa seli zenye saratani.

Hotuba hiyo ya Rais Chavez iliyodumu kwa dakika kumi na tano ililenga kumaliza hofu ya wananchi wa taifa hilo na hakusita kuwaambia kwa sasa anaendelea vizuri huku afya yake ikiimarika.

Rais Chavez ambaye alikasimisha madaraka kwa Makamu wa Rais Elias Jaua amesema amefurahishwa na utendaji kazi wa serikali yake katika muda ambao hakuwepo kwani walikuwa wanawasiliana kwa ukaribu.

Kiongozi huyo akamaliza kwa kuwambia wananchi wa Venezuela kuwa huu si wakati wa majonzi badala yake watumie muda huu kufanyakazi kwa nguvu wakati huu ambapo Kamanda wao anapata ahueni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.