Pata taarifa kuu

China yaahidi hatua madhubuti baada ya ziara ya Makamu wa Rais wa Taiwan nchini Marekani

William Lai, makamu wa rais wa Taiwan, alizuru Marekani. Eneo hili la Asia linadaiwa na Beijing kuwa moja ya maeneo yake tangu mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1949.

Makamu wa Rais wa Taiwan, William Lai akiwasili katika Hoteli ya Lotte huko Manhattan katika Jiji la New York, Marekani, katika picha hii iliyotolewa Agosti 13, 2023.
Makamu wa Rais wa Taiwan, William Lai akiwasili katika Hoteli ya Lotte huko Manhattan katika Jiji la New York, Marekani, katika picha hii iliyotolewa Agosti 13, 2023. via REUTERS - TAIWAN PRESIDENTIAL OFFICE
Matangazo ya kibiashara

ziara ya William Lai, makamu wa rais wa Taiwan, yaikasirisha China. Kisiwa hiki kidogo kinadaiwa na Beijing kuwa moja yamaeneo yake. Hatua hiyo ya Marekani imesababisha China kuchukua "hatua madhubuti na ya nguvu." "China inafuatilia kwa karibu maendeleo ya hali hiyo na itachukua hatua madhubuti kulinda mamlaka yake na uadilifu wa eneo lake," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema katika taarifa yake.

China inaichukulia Taiwan kuwa mojawapo ya majimbo yake, ambayo bado haijaweza kuungana na maeneo mengine ya eneo lake tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China mwaka 1949. Inasema inapendelea Taiwani "kuunganishwa kwa amani". Kwa sasa jimbo hili la Taiwan linatawaliwa na mfumo wa kidemokrasia.

China inaona kuwa ni tishio

China inaona kwa kutoridhishwa na maelewano, katika miaka ya hivi karibuni, kati ya mamlaka ya Taiwan na baadhi ya nchi za Magharibi, hasa Marekani, kuona kuwa ni tishio kwa uadilifu wa eneo lake kwa sababu mikutano hii inaleta aina ya uhalali kwa mamlaka ya Taiwan.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema, "China inapinga vikali aina yoyote ya mawasiliano rasmi kati ya Marekani na Taiwan na inapinga vikali watu wowote wanaotaka kujitenga wanaotetea uhuru wa Taiwan kwenda Marekani."

"Marekani na Taiwan, kwa kula njama, zinaruhusu William Lai kufanya shughuli za kisiasa nchini Marekani kwa kisingizio cha kutokaa nchini humo", hali ambayo "inadhoofisha kwa kiasi kikubwa uhuru na uadilifu wa eneo la China," amesisitiza.

Kulingana na Taiwan, William Lai  'atapiia Marekani - kama rais wa Taiwan Tsai Ing-wen mwanzoni mwa mwezi Aprili - kabla ya kwenda Paraguay kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya, Santiago Pena.

Paraguay ni mojawapo ya nchi za mwisho kuitambua rasmi Taipei. William Lai amerusha picha yake kwenye X (jina jipya la Twitter) siku ya Jumapili, akisema amewasili New York.

Bw. Lai ni mwaniaji wa kumrithi ris wa sasa Tsai Ing-wen. Wote kutoka chama cha wanamgambo wa jadi kwa ajili ya uhuru, wamekuwa wakitukanwa mara kwa mara na Beijing. Jeshi la China liliandaa luteka ya kijeshi siku tatu kuzunguka kisiwa hicho mwezi Aprili kujibu mkutano wa Marekani kati ya spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy na Bi Tsai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.