Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un afanya ziara ya kihistoria nchini Urusi

Kim Jong-un amewasili nchini Urusi, Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imetangaza leo Jumanne Septemba 12, wakati mkutano na Vladimir Putin unatarajia kufanyika. Ziara hii ya kiserikali, ya kwanza nje ya nchi kwa kiongozi wa Korea Kaskazini tangu kuanza kwa janga la UVIKO-19, inaweza kutoa uwezekano wa makubaliano ya silaha kati ya nchi hizo mbili.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akipanda treni kuelekea Urusi, Septemba 10, 2023.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akipanda treni kuelekea Urusi, Septemba 10, 2023. AP - 朝鮮通信社
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Seoul, Nicolas Rocca

Baada ya kutembea kwenye zulia jekundu na kukagua wanajeshi, Kim Jong-un alipanda treni yake maarufu ya kivita, akiwasalimia wanajeshi na watu mashuhuri wa serikali. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa vikitangaza moja kwa moja ziara yake kutoka Pyongyang, ziara aliyoianza siku ya Jumapili. Na kwa sasa atakuwa amewasili nchini Urusi.

Pyongyang na Moscow hazijazungumzia chochote kuhusu ajenda ya mikutano yao, lakini idara ya mawasiliano ya Korea Kaskazini yanatoa baadhi ya habari kuhusiana na ziara ya Kim Jong-un.

Kim Jong-un na Vladimir Putin watakutana wakati wa ziara hii ya kiserikali ya rais huyo, ambayo ni ya kwanza nchini Urusi. Viongozi hao wawili watazungumza kuhusu "masuala nyeti", kama msemaji wa Kremlin alivyotangaza. Haijulikani tarehe au eneo la mkutano huu, ambao utakuwa mkutano wa pili rasmi kati ya Kim Jong-un na Vladimir Putin baada ya mkutano wao mnamo mwaka 2019, katika Mashariki ya Mbali ya Urusi.

Vidokezo vinapendekeza majadiliano kuhusu silaha na teknolojia ya anga

Habari chache zimevuja kuhusu ziara hii adimu ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini nje ya nchi, ikiwa ni ya kumi tangu aingie madarakani mwaka 2011. Lakini picha za ujumbe ktoka Korea Kaskazini kwenye  kituo cha treni zinaonyesha kuwa itakuwa ni suala la silaha, pamoja na teknolojia ya jeshi la majini na la anga. Maafisa wakuu wa kijeshi na waziri wa mambo ya nje wanaonekana kuwa sehemu ya ujumbe huo, pamoja na kamanda wa jeshi la wanamaji na afisa wa mpango wa anga za juu wa Korea Kaskazini. Picha ambazo zinaendana na habari kutoka Washington wiki iliyopita.

"Korea Kaskazini ni wazi iko upande wa China na Urusi. Korea Kaskazini, tangu siku za mwanzo za vita vya Ukraine na uvamizi wa Urusi, imeunga mkono Moscow. Ilikuwa nchi ya kwanza kutambua Jamhuri ya Urusi ya Mashariki mwa Ukraine. Ni nchi ambayo kwa utaratibu, katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, imeunga mkono Urusi na kupiga kura dhidi ya maazimio ya kulaani Moscow,” anaeleza Antoine Bondaz, mkurugenzi wa programu ya Korea katika Wakfu wa Utafiti wa Kimkakati (FRS).

Nchi hizo mbili zinaweza kukubaliana juu ya uanzishwaji wa mazoezi ya pamoja ya jeshi la majini, kwa kubadilishana na kupeleka silaha na risasi kwa Moscow - jambo ambalo Marekani inataka kuepusha kwa gharama yoyote, ambayo inalizungumzia kuwa ni "kosa kubwa". Korea Kaskazini inatafuta msaada wa chakula, lakini pia kupata teknolojia za kujenga manowari zinazotumia nguvu ya nyuklia. Pyongyang inaweza kutafuta usaidizi wa Urusi katika kuweka satelaiti yake mpya kwenye obiti, majaribio mawili ya mwisho ambayo yalishindwa.

Safari za Kim Jong-un nje ya nchi ni chache. (...) Mkutano na Vladimir Putin wenyewe ni hatua muhimu, hata zaidi, katika muktadha wa vita vya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.