Pata taarifa kuu

Washington: Jong Un anataka kukutana na Putin nchini Urusi ili kujadili kuhusu silaha

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anapanga kuzuru Urusi kujadili na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kuhusu mauzo ya silaha kutoka Pyongyang hadi Moscow kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine, Ikulu ya Marekani imesema siku ya Jumatatu.

Kim Jong Un na Vladimir Putin wakati wa ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini huko Vladivostok, Aprili 25, 2019.
Kim Jong Un na Vladimir Putin wakati wa ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini huko Vladivostok, Aprili 25, 2019. AFP - KCNA VIA KNS
Matangazo ya kibiashara

"Kama tulivyosema hapo awali, mazungumzo ya mauzo ya silaha kati ya Urusi na Korea Kaskazini yanaendelea kikamilifu," amesema Adrienne Watson, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la White House.

Na "tunajua kwamba Kim Jong-Un anataka mazungumzo haya yaendelee, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya kidiplomasia katika ngazi ya juu nchini Urusi," ameongeza katika barua pepe kwa vyombo vya habari.

Siku ya Jumatano, msemaji mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa, John Kirby, alielezea kushtushwa na maendeleo ya haraka ya mazungumzo haya juu ya uwasilishaji wa silaha za siku zijazo kutoka Pyongyang kwenda Moscow na alitoa wito kwa serikali ya kikomunisti "kusitisha" majadiliano haya.

Bw Kirby amebainiha kwamba "makubaliano haya yanayoweza kutekelezwa yatawezesha Urusi kupokea kiasi kikubwa" cha silaha, hasa maomu na risasi na silaha za kivita, pamoja na malighafi kwa sekta yake ya ulinzi.

Silaha hizi "zitatumika dhidi ya Ukraine", ameongeza balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield.

- Makampuni vmatatu yachukuliwa vikwazo -

Kwa mujibu wa Gazeti la New York Times, Kim Jong Un anatarajiwa kusafiri hadi Vladivostok, kwenye pwani ya mashariki ya Urusi, kwa kutumia treni ya kivita baadaye mwezi huu kukutana na Vladimir Putin.

Ziara za kiongozi wa Korea Kaskazini nje ya nchi ni nadra. Kando na ziara zake  Singapore na Vietnam mwaka 2018 na 2019 kwa mikutano ya kilele na rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump, Kim Jong Un alifanya ziara nne nchini China. Pia tayari alikutana na Bw. Putin huko Vladivostok mnamo mwaka 2019.

Gazeti la New York Times linabainisha kuwa Bw. Putin anataka kupata makombora ya mizinga na vifaru kutoka Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.