Pata taarifa kuu

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anatarajiwa Vladivostok, Urusi, kwa mkutano na Vladimir Putin

Tangu wiki iliyopita, uvumi umeenea kuhusu uwezekano wa makubaliano ya silaha kati ya Korea Kaskazini na Urusi. Haya yatatangazwa wakati wa mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili. Ikulu ya Kremlin imethibitisha habari hizo ambazo zilikuwa zikisambazwa kwa masharti kwa siku kadhaa katika vyombo vya habari vya Japan na Korea Kusini.

Ujumbe wa Korea Kaskazini unatayarisha treni ya Rais Kim Jong-un, kuelekea Vladivostok nchini Urusi.
Ujumbe wa Korea Kaskazini unatayarisha treni ya Rais Kim Jong-un, kuelekea Vladivostok nchini Urusi. AFP - YURI KADOBNOV
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un atakuwa katika "ziara rasmi" nchini Urusi "katika siku zijazo," Kremlin imesema leo Jumatatu, lakini bado haijatangaza tarehe kamili ya mkutano na Vladimir Putin. Taarifa ya Kremlin inajiwekea kikomo kwa kusema kwamba ziara ya Kim Jong-un ni "kwa mwaliko wa rais wa Urusi" na kwamba marais hao wawili watakuwa na mkutano.

Vyombo vingi vya habari vya Japan na Korea Kusini vimekuwa vikisema kwamba ziara hii ilikuwa ikipangiliwa kwa siku kadhaa, anaripoti mwandishi wetu wa Seoul, Nicolas Rocca. "Treni maalum inayoaminika kuwa inambeba Kim Jong-un inaonekana imeondoka kuelekea Urusi," ndivyo Yonhap, shirika la habari la Korea Kusini, lilivyoripoti habari hiyo. Idara ya kijasusi ya Seoul inabaini kwamba anakoelekea ni Vladivostok ambako Vladimir Putin amepanga ziara ya siku mbili.

Kwa kile ambacho ni ziara rasmi ya kwanza ya kiongozi wa Korea Kaskazini nje ya nchi tangu kuanza kwa janga la Uviko-19, alichagua njia ya jadi ya usafiri wa familia yake: treni. Inaweza kuwa treni ya kifahari ya kivita iliyotumiwa mwaka wa 2019 wakati wa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili. Treni ina mabehewa 90, mifumo ya mawasiliano ya hali ya juu, skrini bapa, vyumba vya mikutano na inaweza hata kubeba helikopta katika tukio la uokoaji.

Kwa usalama zaidi, treni tatu zitafanya kazi kwa wakati mmoja: moja kuangalia hali ya reli, moja itakayombeba Kim Jong-un na washirika wake wa karibu na nyingine itakayobebea wajumbe wengine. Tatizo pekee ni kasi. Miaka minne iliyopita, ilichukua karibu saa ishirini kufika Vladivostok, ingawa ni kilomita 200 tu kutoka Pyongyang. Shirika la habari la Reuters linaelezea kuwepo kwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi  kuliko kawaida, bila ishara nyingine yoyote kuthibitisha ziara ya Kim Jong-un.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.