Pata taarifa kuu

Washington: Urusi na Korea Kaskazini 'zinaendelea kikamilifu' na biashara ya silaha

Mazungumzo juu ya uwasilishaji wa silaha katika siku zijazo kutoka Korea Kaskazini kwenda Urusi "yanaendelea kikamilifu," mshauri wa Ikulu ya White House amesema siku ya Jumatano, ambaye ametoa wito kwa serikali ya Korea Kaskazini "kusitisha" majadiliano haya.

"Urusi inajadili makubaliano ya yanayowezekana na Korea Kaskazini kwa kiasi kikubwa na aina mbalimbali za silaha, kutumia dhidi ya Ukraine," amesema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield huko New York, katika taarifa iliyosomwa kwa niaba ya Marekani, Japan, Korea Kusini na Uingereza.
"Urusi inajadili makubaliano ya yanayowezekana na Korea Kaskazini kwa kiasi kikubwa na aina mbalimbali za silaha, kutumia dhidi ya Ukraine," amesema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield huko New York, katika taarifa iliyosomwa kwa niaba ya Marekani, Japan, Korea Kusini na Uingereza. © Yuri KADOBNOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Makubaliano haya yanayowezekana yatapelekea Urusi kupokea idadi kubwa ya" silaha "za aina kadhaa", hasa risasi, na makombora kwa tasnia ya ulinzi ya Urusi, amesema John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la kitaifa.

"Urusi inajadili makubaliano ya yanayowezekana na Korea Kaskazini kwa kiasi kikubwa na aina mbalimbali za silaha, kutumia dhidi ya Ukraine," ameongeza Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield huko New York, katika taarifa iliyosomwa kwa niaba ya Marekani, Japan, Korea Kusini na Uingereza.

Akilaani tena ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu nchini Korea Kaskazini mwishoni mwa mwezi wa Julai, ambako alihudhuria gwaride la kijeshi pamoja na Kim Jong Un, amebainisha kuwa "ziara hii ilikuwa kiini macho", lakini ililenga "kuishawishi Pyongyang kuuza risasi za kivita”.

"Mkataba kama huo wa silaha utakuwa ukiukaji mkubwa wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa" kwa Korea Kaskazini, amesisitiza, akiitaka Pyongyang "kusitisha" mazungumzo yake na Moscow.

"Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kukiuka maazimio ya Baraza la Usalama kwa vita vyake haramu dhidi ya Ukraine," balozi huyo amekashifu katika taarifa hii ya pamoja, akirejelea hasa shutuma za matumizi ya ndege zisizo na rubani za Iran.

Akielezea mtazamo wa Urusi kama "usiokubalika", amebaini kwamba Marekani ilikuwa ikichukua vikwazo "dhidi ya watu binafsi na mashirika yanayowezesha" makubaliano haya yanayowezekana kati ya Urusi na Korea Kaskazini.

Katikati ya mwezi Agosti, rais wa Urusi Vladimir Putin na Korea Kaskazini walipendekeza kuongezeka kwa ushirikiano, hasa katika nyanja ya ulinzi, kielelezo kipya cha maelewano kati ya maadui hawa wawili wa Marekani tangu kuanza kwa mashambulizi ya Kremlin nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.