Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Biden nchini Vietnam kuimarisha uhusiano wa pande mbili dhidi ya China

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajia kuwasili Vietnam siku ya Jumapili kuchukua hatua mpya katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili, dhidi ya hali ya ushindani na China.

Rais Marekani Joe Biden anajianda kuzuru Vietnam.
Rais Marekani Joe Biden anajianda kuzuru Vietnam. © AP - Abir Sultan
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, ambaye alishiriki wikendi hii katika mkutano wa kilele wa G20 mjini New Delhi, atatua Hanoi siku ya Jumapili kukutana na kiongozi wa Chama tawala cha Kikomunisti, Nguyen Phu Trong.

Atasaini kwenye makubaliano ya "ushirikiano wa kimkakati uliopanuliwa". Hadi sasa, Vietnam imehitimisha tu ushirikiano huo, ambao unaonyesha kiwango cha juu cha ukaribu wa kidiplomasia, na Urusi, India, Korea Kusini na China.

Ikiwa mwangalifu isionekane kuwa inaegemea Washington au Beijing, Hanoi ina wasiwasi kama Marekani juu ya madai ya Beijing katika Bahari ya Kusini ya China - ambako Hanoi ina madai pinzani.

Siku moja kabla ya ziara ya Bw. Biden, Gazeti la New York Times liliripoti kwamba Vietnam ilikuwa ikijadili kwa siri mkataba mpya wa silaha na Urusi licha ya vikwazo vya kimataifa.

Kulingana na hati kutoka Wizara ya Fedha ya Vietnam, iliyotajwa na gazeti hilo la kila siku la Marekani, makubaliano haya yanaweza kufadhiliwa kupitia mradi wa pamoja wa mafuta na Urusi na Vietnam iliyoko Siberia.

Marekani na Vietnam - pia zina uhusiano wa karibu wa kibiashara. Washington inaiona Hanoi kama mshirika muhimu wakati Wamarekani wanatafuta kuanzisha mizunguko ya viwanda duniani ili kutegemea kidogo China.

Siku ya Jumapili, sherehe ya kumkaribisha Joe Biden, hotuba na mkutano na waandishi wa habari wa rais wa Marekani, ambaye siku ya Jumanne alitoa tuzo ya juu zaidi ya kijeshi ya Marekani kwa rubani wa helikopta aliyeokoa wanajeshi wanne wakati wa Vita vya Vietnam, ziko vinaandaliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.