Pata taarifa kuu

Joe Biden aonyesha vipaumbele vyake kabla ya mkutano wa G20 New Delhi

Mkutano wa kundi la nchi zilizostawi kiviwanda duniani (G20i unaanza siku ya Jumamosi Septemba 9 huko New Delhi, nchini India. Rais wa Marekani Joe Biden aliondoka Washington siku ya Alhamisi kuelekea India. Aliondoka akionyesha baadhi ya malengo na vipaumbele

Rais wa Marekani Joe Biden amesafiri kwa ndege kwenda India ambako atashiriki mkutano wa G20 ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Septemba 9, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden amesafiri kwa ndege kwenda India ambako atashiriki mkutano wa G20 ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Septemba 9, 2023. AP - Jess Rapfogel
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Washington, Guillaume Naudin

Joe Biden kwanzaalianza kuonyesha masikitiko yake kabla ya kusafiri kwenda India kushiriki mkutano wa nchi zilizostawi kiviwanda (G20) ambao utafanyika New Delhi Jumamosi Septemba 9. Rais wa Marekani alielezea masikitiko yakekwa kutoweza kukutana na rais wa China Xi Jinping ana kwa ana, ambaye hatahudhuria mkutano huo. Kwa hivyo hakuna mkutano kati ya wawili hawa, kama ilivyo kuwa mwaka jana huko Bali na fursa moja ndogo ya kujaribu kupunguza mvutano kati ya Marekani na Uchina.

Kwa kukosekana kwa Vladimir Putin katika mkutano wa kundi hili mwaka wa pili mfululizo, Joe Biden anaona fursa ya kuwasilisha mtazamo wake kwa washiriki. Washauri wake wanaeleza kuwa rais anaamini muundo wa G20, hata kama wadau muhimu wataususia na kwamba katika hatua hii, taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari sio dhahirikuna uwezekano isitolewi.

Rais wa Marekani anataka kusifu Bidenomics, sera yake ya kiuchumi na kuangazia mbinu yake ya uwekezaji katika miundombinu na kuzingatia masuala ya tabianchi na teknolojia. Ili kufanikisha hili, Marekani inaunga mkono mageuzi ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya mataifa yanayoibukia kiuchumi.

Kuanzia na nchi inayoandaa mkutano huu, India na Waziri Mkuu wake Narendra Modi. Mazungumzo ya nchi mbili unapangwa kabla ya mkutano huo. Marekani inakusudia kuimarisha uhusiano wake na India ili kukabiliana na China, licha ya tofauti zao kuhusu Urusi au haki za binadamu, huku New Delhi ikitaka kwa upande wake kuanzisha jukumu la kimataifa kuwa kwenye mtari wa mbele.

Ikulu ya Marekani pia inafuraha kukaribisha Umoja wa Afrika kama mwanachama kamili kwa mara ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.