Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Ndege nane za kijeshi za China zakaribia maji yanayodhibitiwa na Taiwan

Ndege nane za kijeshi za China zimevuka "mstari wa kati" wa lango la Taiwan, ambao hutenganisha kisiwa hicho na china bara, na kukaribia maji yake.

Ndege za kivita za jeshi la anga la Taiwan F-16 zinaruka kwa mpangilio huku zikidondosha vizuizi vya kuzuia makombora wakati wa siku ya pili ya mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi ya Hankuang. China ilishutumu uamuzi wa Marekani wa kuboresha ndege za kivita za Taiwan F-16.
Ndege za kivita za jeshi la anga la Taiwan F-16 zinaruka kwa mpangilio huku zikidondosha vizuizi vya kuzuia makombora wakati wa siku ya pili ya mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi ya Hankuang. China ilishutumu uamuzi wa Marekani wa kuboresha ndege za kivita za Taiwan F-16. ASSOCIATED PRESS - Wally Santana
Matangazo ya kibiashara

Taiwan inaishi chini ya tishio la mara kwa mara la uvamizi kutoka China, ambayo inakichukulia kisiwa hicho kuwa mkoa ambao bado haujaungana tena na maeneo yake yote tangu kumalizika kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China mnamo 1949, shirika la habari la AFP linakumbusha.

Siku ya Jumamosi, Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema ndege 19, ikiwa ni pamoja na za kivita za kisasa aina ya J-10 na J-16, zimeonekana karibu na eneo lake.

Nane kati ya ndege hizi zilivuka "mstari wa kati wa Mlango-Bahari wa Taiwan", mpaka usioonekana unaotenganisha kisiwa na bara, ukikaribia hadi kilomita 44 kutoka pwani ya Taiwan, Tume imesema katika taarifa.

“Aidha, meli tano za jeshi la wanamaji la China zimefanya doria ya pamoja ya kivita,” imesema wizara hiyo ambayo imebainikwamba inafuatilia kwa karibu hali ilivyo na imepeleka ndege na meli zake za doria katika kukabiliana na tukio lolote la uvamizi.

Uhusiano kati ya Beijing na Taipei umezorota katika miaka ya hivi karibuni na China imeongeza mashambulizi ya angani katika eneo la Utambulisho la Ulinzi wa Anga la Taiwan (ADIZ).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.