Pata taarifa kuu

Taiwan: Makamu wa rais wa sasa ateuliwa kuwa mgombea urais

Chama tawala nchini Taiwan kimemteua Makamu wa Rais William Lai, anayejulikana kwa msimamo wake mkali kwa uhuru wa kisiwa hicho, kuwa mgombea wa uchaguzi wa urais wa 2024 mnamo Jumatano Aprili 12. 

Makamu wa Rais William Lai, anayejulikana kwa msimamo wake mkali kwa uhuru wa Taiwan.
Makamu wa Rais William Lai, anayejulikana kwa msimamo wake mkali kwa uhuru wa Taiwan. © REUTERS - TYRONE SIU
Matangazo ya kibiashara

"Nina heshima na furaha kubwa kupata uteuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kushiriki katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024 na kutekeleza wajibu wa Taiwan wa kulinda Taiwan," Lai amesema katika mkutano wa PDP na waandishi wa habari, shirika la habari la AFP.

Tangazo hilo linakuja baada ya mazoezi makubwa ya kijeshi yaliyofanywa na Beijing kuzunguka Taiwan, ambayo yalisababisha mashambulizi na kuzunguka kisiwa hicho.

Bw. Lai, 63, alikuwa amependekezwa kwa muda mrefu kukubali uteuzi wa chamacha DPP kumrithi Tsai Ing-wen.

Rais wa Taiwan, ambaye muhula wake wa pili wa miaka minne unakaribia kumalizika Mei 2024, hawezi kugombea tena.

William Lai anachukiwa waziwazi na serikali ya Kikomunisti ya China, ambayo inachukulia Taiwan kuwa eneo lake.

William Lai ana msimamo mkali zaidi kuliko Bi Tsai kuhusu suala la uhuru wa Taiwan, hata kama anaona kuwa si lazima kuutangaza rasmi kwa sababu kisiwa "tayari ni nchi huru", kulingana na William Lai.

"Vita haiwezi kuleta amani," alisema mwezi Januari, baada tu ya kuchaguliwa kwake kama kiongozi wa chama cha PDP. Aliwataka WaTaiwan kuungana katika kukabiliana na "utawala wa kimabavu wa China unaopanuka".

"Hatutaacha nafasi yoyote inayotaka kuleta amani," aemongeza, akiomba hata hivyo kufanya kazi na Beijing kuboresha maisha ya wakazi wa pande zote za Mlango wa Taiwan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.