Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

G7 yalenga China, Beijing yaelezea 'kutoridhika kwake'

Taarifa ya viongozi wa G7, ambao kwa sasa wanakutana katika mji wa Hiroshima nchini Japan, inahusu shutuma kadhaa dhidi ya Beijing, zikiwemo masuala ya haki za binadamu, hali ya Bahari ya Kusini ya China na madai ya kuingiliwa.

Rais Joe Biden, wa nne kulia, na viongozi wengine wa G7 wakipiga picha walipokuwa wanatembelea Bustani ya Kumbukumbu ya Amani ya Hiroshima huko Hiroshima, Japani, Ijumaa, Mei 19, 2023, wakati wa Mkutano wa G7.
Rais Joe Biden, wa nne kulia, na viongozi wengine wa G7 wakipiga picha walipokuwa wanatembelea Bustani ya Kumbukumbu ya Amani ya Hiroshima huko Hiroshima, Japani, Ijumaa, Mei 19, 2023, wakati wa Mkutano wa G7. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

China imeeleza Jumamosi, Mei 20 "kutoridhika kwake" baada ya G7 kuchapisha taarifa kwa vyombo vya habari iliyozungumzia kashfa kadhaa juu yake kuhusu Bahari ya Kusini ya China, haki za binadamu au hata kuingilia kati masuala ya nchi wanachama wa G7.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi saba zilizostawi zaidi kiviwanda (Canada, Ufaransa, Marekani, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza) unafanyika tangu Ijumaa katika mji wa Hiroshima nchini Japani, Rais wa Marekani Joe Biden akihudhuria mkutano.

Taarifa ya G7 inatoa wito kwa China "kutofanya shughuli za kuingilia kati masuala ya ndani" ya nchi wanachama wake na inaelezea "wasiwasi" wake kuhusu haki za binadamu "hasa ​​katika majimbo ya Tibet na Xinjiang".

Viongozi wa nchi hizi wanasisitiza "umuhimu wa amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan" na wanasema "wana wasiwasi mkubwa" kuhusu hali ya Bahari ya Kusini ya China, wakiishutumu China kwa "kulazimisha".

Kuhusu Taiwan, wizara ya mambo ya nje inazikosoa nchi za G7 kwa kunyooshea kidole Beijing tu na kutoshtumu vitendo vinavyofanywa na wanaharakati wanaodai kutetea uhuru wa Taiwan.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.