Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Zelensky ashiriki mkutano wa G7 Hiroshima kutetea hoja ya Ukraine

Akisafiri kwa ndege ya Jamhuri ya Ufaransa, rais wa Ukraine amewasili Jumamosi Mei 20 huko Hiroshima, nchini Japan, kushiriki katika mkutano wa kilele wa kundi la nchi zilizostawi zaidi kiviwanda, G7, kwa kukutana na viongozi wa nchi zingine pia, kama vile India na Brazil. Viongozi wa nchi saba zilizoendelea zaidi wameitaka China "kuishinikiza Urusi kusitisha uchokozi wake" dhidi ya Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwasili katika uwanja wa ndege wa Hiroshima kwa ndege ya Ufaransa kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7, Mei 20, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwasili katika uwanja wa ndege wa Hiroshima kwa ndege ya Ufaransa kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7, Mei 20, 2023. © Kyodo News, via AP
Matangazo ya kibiashara

Saa 2:30 asubuhi, saa za Hiroshima, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitua kwenye ndege ya A330 ya Jamhuri ya Ufaransa. Akishuka kwenye ndege peke yake, akiwa amevalia kofia yake ya kahawia, aliwenda haraka ndani ya gari nyeusi ili kufika sehemu kunakofanyika mkutano wa G7: Hoteli ya Grand Prince huko Hiroshima, ambako wajumbe kutoka G7 wanakutana, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Hiroshima, Vincent Souriau.

Katika Twitter, mara moja rais wa Ukraine amebaini kuwa amani iko "karibu" kufuatia mkutano huu wa kilele.

Rais wa Ukraine atakutana na vongozi mbalimbali. Kwanza, na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Kwa sababu Volodymyr Zelensky anakuja kutafuta uungwaji mkono wa nchi zilizoalikwa katika mkutano wa G7, hasa India na Brazili, ambazo bado hazijachukua msimamo thabiti kuhusu vita vya Ukraine na bado zinakuza uhusiano wao wa karibu na Urusi.

India itafanya "kila linalowezekana" kusuluhisha mzozo wa Urusi na Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi moja kwa moja  kwa mara ya kwanza tangu nchi yake kuvamiwa na Urusi, uvamizi ambao New Delhi imekataa kuukashifu.

Kando ya mkutano G7, mkuu wa serikali ya India amehakikisha kwamba New Delhi itafanya "kila linalowezekana" kupata suluhisho la mzozo wa Urusi na Ukraine: "Ninaelewa kikamilifu mateso yako na mateso ya watu wa Ukraine. Ninaweza kukuhakikishia kwamba kusuluhisha [vita], India na mimi binafsi tutafanya kila tuwezalo. »

Ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya Telegram ya Volodymyr Zelensky ulisema "ameishukuru India kwa msaada wake kwa uadilifu wa eneo na uhuru" wa Ukraine, "hasa ​​mbele ya mashirika ya kimataifa". Rais wa Ukraine pia amemshukuru Narendra Modi kwa misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa nchi yake iliyokumbwa na vita na kutoa wito kwa India kushiriki katika utekelezaji wa "mchakato wa amani ya kudumu" uliyoandaliwa na Ukraine.

Mkutano wa faragha pia umepangwa jioni na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye ametoa wito siku ya Jumamosi kwamba uwepo wa mwenzake wa Ukraine katika mkutano wa G7 "unaweza kubadilisha hali ya mambo" kwa Ukraine: "Ni fursa ya kipekee" kwa Volodymyr Zelensky kubadilishana na washirika wake wa G7, lakini pia kusihi sababu ya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi na viongozi wa nchi za Kusini walioalikwa kwenye mkutano huo, amebainisha rais wa Ufaransa. "Nadhani inaweza kubadilisha hali ya mambo," ameongeza.

Mkutano mwingine utafanyika na Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye ametoa idhini ya kuipa Ukraine ndege ain ya F16, uamuzi ambao Volodymyr Zelensky alielezea mara tu alipoutangaza Ijumaa Mei 19 kama "wa kihistoria".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.