Pata taarifa kuu

India: Kiongozi wa upinzani Rahul Gandhi afukuzwa katika Bunge

Kiongozi wa upinzaji Rahul Gandhi amefukuzwa hivi punde katika Baraza la Bunge nchini India, siku moja baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kashfa. Mgombea wa zamani kwenye nafasi ya Waziri Mkuu sio mjumbe tena wa Baraza la Bunge, wakati alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani. Hatu hiyo ni pigo kwa Chama cha Congress, ambacho huona nafasi zake kupungua kabla ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka ujao.

Rahul Gandhi, Januari 23, 2023. "Ni siku ya giza kwa demokrasia ya India," kiongozi wa vuguvugu la vijana wa chama cha Congress, Srinivas Bhadravathi Venkata ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Rahul Gandhi, Januari 23, 2023. "Ni siku ya giza kwa demokrasia ya India," kiongozi wa vuguvugu la vijana wa chama cha Congress, Srinivas Bhadravathi Venkata ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. AP - Channi Anand
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu nchini India, Sébastien Farcis

Ni pigo kubwa kwa chama cha Congress: Rahul Gandhi alikuwa amemaliza ziara ya miezi mitano nchini kote ili kurekebisha picha yake na ile ya chama chake; Mwana na mjuu wa Waziri Mkuu ana jina ambalo linavutia wapiga kura na liliwehusu chama cha Congress kutarajia kuwakilisha njia mbadala katika uchaguzi wa mwaka ujao.

BJP imepiga sehemu nyeti

Sasa, chama cha Congress kimepoteza bahati, kwa mujibu wa Sudab Bhai, profesa katika kitivo cha sayansi ya kisiasa: "Chama cha BJP hakijapoteza nafasi kwa kuwachapa wapinzani wake, na chama hiki kimepiga vya kutosha kwa kutumia mahakama katika nchi wanayodhibiti. Uwezo kwamba Congress kitashinda uchaguzi hiyo ni ndoto ya mwendawazimu, lakini inaweza ikafikia. Congress inaweza kuwa haijafahamika, na kwa vile upinzani umegawanyika, kuna nafasi nzuri kwamba Narendra Modi atachaguliwa tena mwaka ujao. "

Mlipuko wa mashtaka

Mashitaka ya mamlaka dhidi ya upinzani yamelipuka katika miaka ya hivi karibuni, na kupeleka viongozi wake wengi gerezani au kuwalazimisha kujiunga na BJP. Rahul Gandhi bado ana nafasi nyembamba ya kurudi bungeni ikiwa mahakama ya juu kitafuta hukumu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.