Pata taarifa kuu

India na China, nchi mbili zenye nguvu barani Asia kati ya mashindano na kutegemeana

Wakati Kongamano la 20 la Chama cha Kikomunisti nchii China (CCP) likifunguliwa, tuangalie tena uhusiano kati ya nchi mbili zenye nguvu katika bara la Asia, India na China. Uhusiano wa kutegemeana ulioharibiwa na migogoro ya kijeshi na ushindani wa kibiashara na kidiplomasia.

Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano wa kilele wa kimataifa Septemba 4, 2017.
Rais wa China Xi Jinping (kushoto) na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano wa kilele wa kimataifa Septemba 4, 2017. REUTERS/Kenzaburo Fukuhara
Matangazo ya kibiashara

Hata kama nchi hizo mbili ziliangamizwa na ukoloni na kuweza kudai kuwa hazifungamani, uhusiano wao umekuwa na migogoro kwa muda mrefu. Baada ya uhuru mnamo 1947, India na China zilishindwa kukubaliana juu ya mipaka yao katika Milima ya Himalaya. Hii ilisababisha, mwaka 1962, kwa vita na maelfu ya vifo kwa ajili ya udhibiti wa Aksai Chin, eneo la jimbo la India la Arunachal Pradesh ambalo China inalichukulia kuwa lake. Miaka michache kabla, India iliiruhusu China kuivamia Tibet, lakini iliamua kupokea wakimbizi na serikali ya Dalai Lama, sera ambayo bado ipo na inaikasirisha Beijing.

Tangu Narendra Modi aingie madarakani, mapigano kadhaa yametokea, haswa katika bonde la barafu la Galwan mnamo 2020, ambapo mapigano yalisababisha vifo vya askari kadhaa. Hali ya mpaka inasalia kuwa ya wasiwasi na vikosi viko macho kwa pande zote mbili. India inaishutumu China kwa kujenga miundombinu haramu mjini Arunachal Pradesh. Hatimaye, India pia ni mwanachama wa muungano wa Indo-Pacific, ikiwa upande wa Marekani, hali ambayo inapingana na China  juu ya suala lenye utata la Taiwan.

Suala muhimu la kutegemeana

Ushindani huo pia unaripotiwa katika nyanja ya kibiashara, kwani hakuna kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia inayetaka kushiriki katika vita. Hivi ndivyo Narendra Modi alivyohamisha mzozo huo kwa kupiga marufuku programu nyingi za China, pamoja na TikTok maarufu sana, baada ya mapigano ya 2020. Tangu kuchaguliwa tena mnamo 2019, Waziri Mkuu wa India ameweka jukumu lake chini ya ishara ya kujitosheleza kwa India. Maneno ambayo anatumia mara kwa mara akimaanisha India inategemea sana China, hasa kwa vifaa vya umeme na elektroniki, malighafi na mbolea.

Kwa kweli, nakisi ya biashara kati ya nchi hizo mbili imeongezeka hivi karibuni. Makadirio ya hivi punde yanaonyesha kuwa India inaagiza euro bilioni 77 katika bidhaa na huduma kuliko inavyosafirisha kwenda China. Kwa hivyo nyuma ya matamko ya kivita, kila mtu anajua kwamba anamuhitaji mwingine, India kwanza kabisa.

Mazungumzo ya kidiplomasia ya mara kwa mara

Mnamo 2019, Xi Jinping alifanya ziara ya hali ya juu nchini India. Mnamo 2021, alishiriki, katika mkutano wa kilele wa BRICS ulioandaliwa New Delhi. Wanadiplomasia hufanya mazungumzo mara kwa mara kuhusu migogoro ya mipaka na masuala ya biashara. 

Hata hivyo, hali imebadilika tangu vita vya Ukraine. India, ambayo inakataa kupinga Urusi, mshirika wa kihistoria wa kijeshi, inajikuta ikijizuia pamoja na China wakati wa kupiga kura juu ya maazimio katika Umoja wa Mataifa. Ili kutojipata kutengwa, China inanufaika na msimamo huu wa India wa kutoegemea upande wowote. Kwa hivyo inaweza kufanya ishara za uwazi, ambazo itabidi zijulikane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.