Pata taarifa kuu

Ufilipino: Idadi ya watu waliofariki kutokana na Kimbunga Nalgae yaendelea kuongezeka

Idadi ya watu waliokufa kutokana na Kimbuga Nalgae kilichoikumba Ufilipino imeongezeka Jumatatu, Oktoba 31, na kufikia watu 98 waliokufa, huku miili zaidi ikipatikana.

Idadi ya watu waliokufa kutokana na Kimbunga Nalgae kilichoikumba Ufilipino imeongezeka Jumatatu, Oktoba 31, na kufikia watu 98 waliokufa, huku miili zaidi ikipatikana.
Idadi ya watu waliokufa kutokana na Kimbunga Nalgae kilichoikumba Ufilipino imeongezeka Jumatatu, Oktoba 31, na kufikia watu 98 waliokufa, huku miili zaidi ikipatikana. REUTERS - LISA MARIE DAVID
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa wahanga walikufa katika maporomoko ya ardhi na mafuriko Ijumaa ya wiki iliyopita huko Mindanao, kisiwa cha kusini mwa nchi hiyo. Kimbunga hiki kilipiga kisiwa kikuu cha Luzon usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, na kusababisha umeme kukatika. Mji mkuu wa Manila na miji jirani imekumbwa na mafuriko makubwa.

Idadi ya wahanga inaweza kuongezeka tena, idara ya kudhibiti majanga ya asili imerodhesha watu 63 waliotoweka katika ripoti yake ya hivi punde, huku watu kadhaa wakijeruhiwa. Mamlaka za eneo hilo zimetangaza kwamba wamesitishana "operesheni ya utafutaji na uokoaji na kuanzisha operesheni ya kutoa miili kwenye maki kwa sababu hakuna matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai".

Vimbunga na dhoruba 20 kwa mwaka

Wastani wa vimbunga na dhoruba 20 huikumba Ufilipino kila mwaka, na kuua watu na mifugo maene kinapopita, na kuharibu mashamba, nyumba, barabara na madaraja, ingawa kusini huathiri mara chache. Katika miaka ya hivi karibuni, maporomoko ya ardhi na mafuriko makubwa katika maeneo ya milimani yaliyoathiriwa na ukataji miti imekuwa miongoni mwa matokeo mabaya zaidi ya dhoruba nchini Ufilipino.

Ni dhoruba ya tatu mbaya kupiga Ufilipino mwaka huu. Mwishoni mwa mwezi wa Septemba, Kimbunga Noru kiliua takriban watu 10, wakiwemo waokoaji watano. Kimbunga cha kitropiki cha Megi, kilichoikumba nchi hiyo mwezi Aprili, kiliua takriban watu 148 na kusababisha maporomoko makubwa ya udongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.