Pata taarifa kuu

Ufilipino: Kimbunga Nalgae chasababisha mafuriko na matope na kutishia Manila

Kimbunga cha Tropiki Nalgae, ambacho kimeikumba Ufilipino, sasa kinatishia mji mkuu wa Manila baada ya kuua takriban watu 45 kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi katika kisiwa hicho.

Kimbunga cha kitropiki cha Nalgae, kilichopiga Ufilipino Jumamosi (tarehe 28 Oktoba), sasa kinatishia mji mkuu wa Manila baada ya kuua takriban watu 45 kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi katika visiwa hivyo.
Kimbunga cha kitropiki cha Nalgae, kilichopiga Ufilipino Jumamosi (tarehe 28 Oktoba), sasa kinatishia mji mkuu wa Manila baada ya kuua takriban watu 45 kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi katika visiwa hivyo. via REUTERS - PHILIPPINE COAST GUARD
Matangazo ya kibiashara

Kimbunga cha Nalgae, kilichootarajiwa tangu siku ya Alhamisi, hatimaye kimepiga kisiwa kikuu cha Ufilipino alfajiri ya Jumamosi, kikiambatana na upepo unaokwenda kilomita 95 kwa saa na mvua kubwa. Maji ya mafuriko yamevamia miji na vijiji kadhaa kwenye kisiwa cha Mindanao, yakiwa yamesomba miti, mawe na matope maeneo kilipokuwa kikipita. Nyumba 500 hivi zimeharibiwa.

Kuanzia sasa, Nalgae pia inaweza kuathiri mji mkuu wa Manila na wakazi wake milioni 13, imeonya mamlaka ya hali ya hewa nchini Ufilipino ambayo inaonya juu ya "mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yanayosababishwa na mvua". Zaidi ya watu 7,000 wamehamishwa kabla ya kuwasili kwa kimbunga hiki na timu 5,000 za waokoaji zimehamasishwa, mamlaka pia imetangaza.

Kimbunga cha tatu  kibaya kwa mwaka mmoja

Wastani wa vimbunga na dhoruba ishirini huikumba Ufilipino kila mwaka, na kuua watu na mifugo pote vinapopita, na kuharibu mashamba, nyumba, barabara na madaraja, ingawa kusini huathiri mara chache. Kadiri sayari inavyoathiriwa na ongezeko la joto duniani, dhoruba na vimbunga vinazidi kuwa na nguvu zaidi, wanasayansi wanaonya.

Ni kimbunga cha tatu kibaya kupiga Ufilipino mwaka huu. Mwishoni mwa mwezi Septemba, Kimbunga Noru kiliua takriban watu 10, wakiwemo waokoaji watano. Kimbunga cha kitropiki cha Megi, kilichoikumba nchi hiyo mwezi Aprili, kiliua takriban watu 148 na kusababisha maporomoko makubwa ya ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.