Pata taarifa kuu

Japani: Serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu 'Kanisa la Umoja', Moon

Nchini Japani, uchunguzi wa serikali utaanza kuhusu Kanisa la Muungano, linalojulikana zaidi kama dhehebu la Mwezi (Moon). Iliagizwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida baada ya mauaji  ya Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe mwezi Julai, ambayo yalifichua uhusiano wa muda mrefu kati ya serikali na kundi hili.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mnamo Oktoba 17, 2022 huko Tokyo.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mnamo Oktoba 17, 2022 huko Tokyo. © Keisuke Hosojima/Kyodo News via AP
Matangazo ya kibiashara

Hata baada ya kuuawa kwa Shinzo Abe, Waziri Mkuu Fumio Kishida alikataa kufungua uchunguzi kuhusu shughuli za kikundi cha Mwezi huko Japan, anakumbusha mwandishi wetu wa Tokyo, Frédéric Charles. Kwa miongo miwili iliyopita, mtandao wa wanasheria wa waliokuwa waumini wa Kanisa la Muungano wamekuwa wakitoa wito kwa chama tawala cha Conservative kuvunja uhusiano wake na kundi hilo la kidini. Muuaji wa Shinzo Abe, Tetsuya Yamagami, aliamini kuwa waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa karibu na dhehebu alililoshtumu kuhusika na machafuko ambayo familia yake ilikabili, baada ya mama yake kuchangia pesa nyingi kwake. Inaaminika kuwa Yamagami alimlenga Abe kwa sababu alikuwa na uhusiano na kundi hilo.

Tangu miaka ya 1960, Chama cha Conservative kilitumia wafuasi wa dhehebu hilo wakati wa kampeni za uchaguzi. 

Akihutubia Bunge siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu alielekeza kwa “wahanga wengi” wa Kanisa hili na makundi yanayohusiana, ambao waliishia katika umaskini au kukabiliwa na matatizo makubwa ya kifamilia. Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameamuru kufunguliwa kwa uchunguzi. Serikali pia inataka kurekebisha baadhi ya sheria ili kurahisisha kufuta kandarasi, na "itaimarisha mipango ya kuzuia unyanyasaji wa watoto na kuwasaidia watoto wa wafuasi katika elimu na ajira zao," waziri mkuu amesema.

"Kanisa la Muungano” ni nini?

Uainishaji wa "Kanisa la Muungano" hutofautiana kati ya wafuasi wake na wapinzani, wakati kwenye tovuti yake rasmi inajifafanua kuwa "vuguvugu la kidini na chama cha kidini kisicho na faida", wengine wanaliainisha kama "dhehebu hatari la kidini".

Vuguvugu hilo lilianzishwa mwaka wa 1954 na Sun Myung Moon (1920-2012), kama "Kikundi cha Roho Mtakatifu cha Kuunganisha Wakristo Ulimwenguni", lakini jina lake limebadilika kwa miaka mingi na kuwa leo "Umoja wa Familia kwa Amani ya Ulimwenguni." na Umoja", na inatumika hasa Korea Kusini na Japani na Marekani. Kundi hilo limepewa jina la utani "Moniz" kutokana na neno la Kiingereza linalotumiwa kuwaelezea wafuasi wa Mwezi.

Kulingana na Encyclopedia Britannica, wafuasi wa vuguvugu hilo wanaamini kwamba Muumba alitaka mwanadamu ajionee furaha ya upendo. Lakini Adamu na Hawa walishindwa kutimiza lengo hilo, na upendo wa ubinafsi uliipotosha dunia. Muumba alitaka kurejesha kile kilichoharibiwa, kwa kutuma waokoaji wengi kwa wanadamu, kati yao Kristo, ambaye hangeweza kukamilisha utume wake kwa sababu hakuoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.