Pata taarifa kuu
JAPAN

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe apigwa risasi, ajeruhiwa vibaya

Nchini Japan, aliyekuwa Waziri Mkuu Shinzo Abe amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya  alipokuwa katika mkutano wa siasa katika mji wa Nara Magharibi mwa nchi hiyo.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe baada ya kupigwa risasi Julai 8 2022 akiwa kwenye mkutani wa siasa.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe baada ya kupigwa risasi Julai 8 2022 akiwa kwenye mkutani wa siasa. AP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, Abe, alipigwa risasi mara mbili mgongoni na kuanguka chini, huku mshukiwa akikamatwa.

Aidha, ripoti zinasema kuwa hali yake ni mbaya na amekimbizwa hospitalini, huku kukiwa na ripoti kuwa haoneshi dalili za kuzinduka.

Abe, aliyeongoza Japan kwa kipindi kirefu kati ya mwaka 2012 hadi 2020, alipigwa risasi wakati akitoa hotuba ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa wabunge siku ya Jumapili.

Shambulio hilo dhidi ya mwanasiasa huyo maarufu mwenye umri wa miaka 67, limewashangaza wengi katika nchi hiyo ya barra Asia ambayo haina historia ya kushuhudia matukio kama haya kufuatia uwepo wa sheria kali za kudhibiti umiliki wa silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.