Pata taarifa kuu

Japan: mkuu wa polisi wa kitaifa ajiuzulu baada ya kuuawa kwa Shinzo Abe

Mkuu wa polisi wa kitaifa wa Japan, Itaru Nakamura, alitangaza siku ya Alhamisi kwamba amewasilisha ombi la kujiuzulu baada ya kukiri kushindwa katika ulinzi wa Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe, ambaye aliuawa Julai 8 wakati wa kampeni ya uchaguzi. 

Shinzo Abe aliaga dunia kutokana na majeraha yake baada ya kulengwa kwa risasi Julai 8, wakati wa kampeni ya uchaguzi katika eneo la Nara (magharibi mwa Japani).
Shinzo Abe aliaga dunia kutokana na majeraha yake baada ya kulengwa kwa risasi Julai 8, wakati wa kampeni ya uchaguzi katika eneo la Nara (magharibi mwa Japani). REUTERS - KIM KYUNG-HOON
Matangazo ya kibiashara

"Tumeamua kupanga upya timu yetu na kuanza upya kuhusiana na misheni zetu za usalama, na ndiyo maana nimejitolea kujiuzulu," Bw. Nakamura amesema katika mkutano na wanahabari.

Shinzo Abe aliaga dunia kutokana na majeraha yake baada ya kulengwa kwa risasi Julai 8, wakati wa kampeni ya uchaguzi katika eneo la Nara (magharibi mwa Japani).

Mtu anayeshukiwa na mauaji ya Shinzo Abe, Tetsuya Yamagami, alikamatwa katika eneo la tukio na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili hadi mwisho wa mwezi Novemba. Aliwaambia polisi kwamba alimlenga kiongozi huyo wa zamani kwa sababu ya uhusiano wake na Kanisa la Muungano, ambalo pia linajulikana kama dhehebu la Mwezi, ambalo analichukia.

Siku moja baada ya kuuawa kwa Shinzo Abe, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Nara Tomoaki Onizuka alikiri kwamba "ilikuwa jambo lisilopingika kwamba kumekuwa na matatizo ya ulinzi na hatua za usalama" za waziri mkuu huyo wa zamani. “Ni dharura tufanye uchunguzi wa kina ili kufafanua kilichotokea,” aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.