Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Coronavirus: Australia kuendelea kutumia chanjo ya AstraZeneca

Australia haina mpango wa kusitisha utumiaji wa chanjo dhidi ya Corona iliyotengenezwa na maabara ya AstraZeneca, mamlaka nchini humo imesema leo Jumanne, wakati nchi kadhaa za Ulaya pamoja na Ufaransa zilisitisha utumiaji wa chanjo hiyo kwa hofu ya kusababisha madhara.

Nchini Australia, huko Melbourne, wafanyikazi wako hatarini zaidi kwa kuambikizwa virusi vya Corona, kulingana na uchunguzi (picha ya kumbukumbu).
Nchini Australia, huko Melbourne, wafanyikazi wako hatarini zaidi kwa kuambikizwa virusi vya Corona, kulingana na uchunguzi (picha ya kumbukumbu). William WEST / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wakati shirika la madawa la Umoja wa Ulaya (EMA) likiendelea na uchunguzi, Australia inatangaza kuwa chanjo ya AstraZeneca dhidi ya COVID-19 ni yenye ufanisi mkubwa kwa kukabiliana dhidi ya COVID-19 na inapaswa kuendelea kutumiwa," amesema mkurugenzi wa afya nchini Australia.

Katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe, Paul Kelly ameongeza kuwa serikali itaendelea kuwa na imani na chanjo hiyo licha ya kwamba hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa inasababisha kuganda kwa damu. Amesema, hata hivyo, kwamba madhara yanayoshukiwa yatachunguzwa "kama hatua ya tahadhari".

Baadhi ya nchi za Ulaya zatumia chanjo ya AstraZeneca

Nchi zingine kadhaa, pamoja na Uingereza na Poland, zinaendelea kutumia chanjo ya AstraZeneca.

Watu milioni 25 wa Australia watapokea dozi za chanjo kutoka AstraZeneca, maabara ambayo ilisaini mkataba na Canberra wa karibu dozi milioni 54 - ambapo dozi milioni 50 zinatarajiwa kutengenezwa nchini humo mwishoni mwa mwezi Machi.

Kampeni ya kutoa chanjo nchini Australia ilianza mwezi uliopita, siku kadhaa baada ya nchi nyingi za Ulaya kuanza zoezi hilo. Chanjo ya AstraZeneca ilianza kutumiwa Australia tangu wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.