Pata taarifa kuu
UTURUKI-HAKI

ECHR: Ankara yahukumiwa kwa kuwaweka kizuizini mahakimu 427

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imeihukumu Uturuki kwa kuwaweka kizuizini kiholela mahakimu 427 baada ya kushindwa kwa mapinduzi ya mwezi Julai 2016;

Baada ya mapinduzi yaliyofeli ya Julai 2016, mamlaka ya Uturuki ilianzisha operesheni ya kuwakamata wafuasi wa Fethullah Gülen, adui mkubwa wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (picha yetu).
Baada ya mapinduzi yaliyofeli ya Julai 2016, mamlaka ya Uturuki ilianzisha operesheni ya kuwakamata wafuasi wa Fethullah Gülen, adui mkubwa wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (picha yetu). Ozan KOSE AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kwa kauli moja, majaji wa Ulaya wamebaini kwamba Ankara ilikiuka "haki ya uhuru", iliyohakikishwa na Mkataba wa Ulaya wa Haki za binadamu, kwa kuwaweka mahakimu 427 kizuizini kabla ya kesi. Majaji hawa na waendesha mashtaka ambao walifanya kazi katika maeneo mengi ya mamlaka, ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Uchunguzi na Mahakama Kuu ya Utawala, walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa "tuhuma za kuwa katika vuguvugu la FETO", inaeleza ECHR katika taarifa. Katika istilahi za mamlaka ya Uturuki, FETO ni kifupi cha "kundi la Kigaidi la wafuasi wa Fethullah" Gülen, anayeshutumiwa kupanga jaribio la mapinduzi.

Mahakama iliamuru Ankara kulipa euro 5,000 kwa kila hakimu kwa kutowatendea haki. Baada ya mapinduzi yaliyofeli ya Julai 15, 2016, mamlaka ya Uturuki ilianzisha operesheni ya kuwakamata wafuasi wanaodaiwa kuwa wa Fethullah Gülen, adui mkubwa wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, lakini pia dhidi ya wapinzani wa Kikurdi, wanajeshi, wasomi au waandishi wa habari, wakiwakamata makumi ya maelfu ya watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.