Pata taarifa kuu

Uturuki yaiuzia Ethiopia ndege zisizo na rubani

Kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, Ankara imeikabidhi serikali ya Ethiopia ndege zisizo na rubani, ambayo imekuwa ikiendesha vita katika jimbo la Tigray dhidi ya waasi kwa karibu mwaka mmoja.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisafiri kwenda kwenda Sochi Septemba 29, 2021 kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisafiri kwenda kwenda Sochi Septemba 29, 2021 kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin. AFP - VLADIMIR SMIRNOV
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo wa kutuma ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki kwenda Ethiopia ulifanyika wakati wa mkutano kati ya Abiy Ahmed na Recep Tayyip Erdogan katika mji mkuu wa Uturuki, mwezi wa Agosti mwaka huu. Ndege hizi zisizo na rubani zinaweza kutumika hivi sasa kupigana na waasi katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Kufufuliwa kwa uhusiano kati ya Addis Ababa na Ankara hivi karibuni kunatia mashaka waangalizi wengi. Kwanza ni kwa sababu ya ziara ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed nchini Uturuki, ambapo viongozi hao walitia saini mikataba ya ushirikiano wa kijeshi na uchumi. Siku chache kabla ya ziara hii rasmi, Ethiopia iliamua ghafla kufunga shule kumi na moja za vuguvugu la Hizmet la Fetullah Gulen, adui namba moja wa rais wa Uturuki.

Leo, vyanzo kadhaa vya kidiplomasia vinabaini kwamba kufufuliwa kwa uhusiano kati ya nchi hii mbili kunajumuisha kutumwa kwa ndege zisizo na rubani kutoka Uturuki kwenda Ethiopia. Ndege hizo aina ya Bayraktar TB2 ambazo zilitumiwa wakati wa mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia mwaka jana. Kulingana na waasi wa TPLF huko Tigray, jeshi la shirikisho limekuwa likitumia ndege zisizo na rubani katika vita tangu wiki iliyopita kaskazini mwa Ethiopia, ingawa hakuna picha zilizovuja hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.