Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Uturuki yadai kutokuwa na imani na mabalozi kumi wanaomuunga mkono Osman Kavala

Nchini Uturuki, mabalozi wa nchi kumi za Magharibi ambao wiki hii walitaka kuachiliwa kwa mfanyabiashara na mtaalamu wa uhisani Osman Kavala watatangazwa na Recep Tayyip Erdogan kuwa hawatakiwi kuendelea kuhudumu kwa niaba ya nchi zao nchini Uturuki.

Osman Kavala, mwenye umri wa miaka 64, anazuiliwa nchini Uturuki bila kuhukumiwa tangu mwaka 2017.
Osman Kavala, mwenye umri wa miaka 64, anazuiliwa nchini Uturuki bila kuhukumiwa tangu mwaka 2017. Handout Anadolu Culture Center/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza Jumamosi kwamba alikuwa ameamuru wizara yake ya mambo ya nje kutangaza kutokuwa na imani na mabalozi wa Marekani, Uholanzi, Ufaransa, Finland, Sweden, Norway, New Zealand, Denmark, Canada na Ujerumani, ambao wanatakiwa kuondoka nchini Uturuki.

"Nilimwagiza Waziri wetu wa Mambo ya nje kusuluhisha haraka iwezekanavyo tangazo la mabalozi hawa kumi kama hawatakiwi kuendeklea kuhudumu kwa niaba ya nchi zao nchini Uturuki", amebaini rais Erdogan wakati wa ziara yake katikati mwa Uturuki, bila hata hivyo kutoa tarehe maalum.

"Mnafikiri mko wapi? Hapa ni Uturuki, sio taifa la kikabila, ”rais wa Uturuki ameambia umati wa wafuasi wake, mwandishi wetu huko Istanbul, Anne Andlauer ameripoti. Kabla ya kuongeza, akiwaambia mabalozi: "Ikiwa hawaelewi Uturuki, wataiacha. "

Katika barua ya pamoja, mabalozi wa nchi hizi kumi walitoa wito wiki hii ili kuachiliwa mara moja kwa Osman Kavala, ambaye amekuwa hasimu wa serikali na kuzuiliwa bila hatia tangu Oktoba 18, 2017. Anatuhumiwa kufadhili maandamano dhidi ya serikali huko Gezi Park mnamo mwaka 2013 na kwa kuhusika katika mapinduzi yaliyotibuliwa ya 2016, madai ambayo anakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.