Pata taarifa kuu
UTURUKI-ULINZI

Uturuki kuanzisha mazungumzo na Marekani kuhusu ndege za F-16

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa tangazo hilo Jumapili wakati Uturuki iliondolewa kwenye mpango wa ndege za kivita za F-35 za Marekani.

"Tulisema kwamba tutachukua hatua zote muhimu kukidhi mahitaji ya ulinzi ya nchi yetu," amebaini Recep Tayyip Erdogan.
"Tulisema kwamba tutachukua hatua zote muhimu kukidhi mahitaji ya ulinzi ya nchi yetu," amebaini Recep Tayyip Erdogan. AFP - ADEM ALTAN
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa Jumapili, Oktoba 17, na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Amesema nchi yake kwa sasa inafanya mazungumzo na Marekani juu ya kupatikana kwa ndege za kivita za F-16. Ikifahamika kuwa Uturuki hapo awali ilitengwa kutoka kwa mpango wa ndege za kivita za Marekani F-35 mnamo 2019, baada ya kununua mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi S-400. Kama ukumbusho, wakati ilikuwa mshirika katika mpango wa ndege za kijeshi za Marekani, Uturuki ilitarajia kupata karibu ndege 100 za kivita.

Ankara sasa inadai fidia kwa kufukuzwa kwake kutoka mpango wa Marekani, hasa kwa malipo ya dola bilioni 1.4 zilizolipwa kabla ya kutengwa.

Kujibu "Mahitaji ya Ulinzi" ya Uturuki

"Tulizungumzia suala hili katika mazungumzo yetu. Tunaona umuhimu wa mazungumzo ili kupata suluhisho la tatizo hili, ”Recep Tayyip Erdogan amewaambia waandishi wa habari Jumapili hii kwenye uwanja wa ndege huko Istanbul, kabla ya kuanza ziara yake barani Afrika. Mpango wa Uturuki wa kununua ndege za F-16 "bila shaka unahusishwa na tatizola ndege ain ya F-35," amesema, akiongeza kuwa Marekani ilitoa pendekezo kwa Uturuki kuuza ndege aina ya F-16 ili kuboresha vyombo vyake vya angani.

"Tulisema kwamba tutachukua hatua zote muhimu kukidhi mahitaji ya ulinzi ya nchi yetu," amebaini Recep Tayyip Erdogan, na kuongeza kuwa Uturuki ilikuwa ikifanya kazi ili kuboresha ndege zake za kivita. Uuzaji wa ndege za F-16, hata hivyo, unatarajiwa kupitishwa na Bunge la Marekani ambalo uhasama dhidi ya Uturuki unaongezeka.

Mwezi uliopita, Recep Tayyip Erdogan alibaini kwamba Uturuki bado ilikuwa na mipango ya kupata kundi la pili la mifumo ya ulinzi ya makombora ya S-400 kutoka Urusi, hali ambayo Marekani ilionya kuhusu hatari za 'kuzorota zaidi kwa uhusiano wao wa nchi hizi mbili .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.