Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Uturuki yafanya mazungumzo na maafisa wa Taliban

Uturuki, ambayo ina mpango wa kukamilisha zoezi la kuondoa vikosi vyake vya mwisho katika uwanja wa ndege wa Kabul ndani ya saa chache zijazo, imefanya mazungumzo na Taliban katika mji mkuu wa Afghanistan, kulingana na rais Recep Tayyip Erdogan.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza kuwa mamlaka ya Uturuki imekuwa na mazungumzo marefu na maafisa wa Taliban siku moja baada ya shambulio karibu na uwanja wa ndege wa Kabul.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza kuwa mamlaka ya Uturuki imekuwa na mazungumzo marefu na maafisa wa Taliban siku moja baada ya shambulio karibu na uwanja wa ndege wa Kabul. AFP - ADEM ALTAN
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki ameongeza kwamba Taliban imeipendekezea Ankara kusimamia uwanja wa ndege baada ya kuondoka kwa vikosi vya Marekani. Rais wa Uturuki amesema bado hajachukuwa uamuzi. Kutokana na hatari iliyopa, mamlaka ya Uturuki inasita.

Uturuki italazimika kuchukuwa uamuzi ambao ni mgumu. Hivi ndivyo Recep Tayyip Erdogan amedokeza, akithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba Taliban imeiomba nchi yake msaada katika kusimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kabul baada ya vikosi vya Marekani kuondoka. Mazungumzo ya awali yamefanyika kwa zaidi ya saa tatu katika sehemu ya kijeshi ya uwanja wa ndege, ambapo ubalozi wa Uturuki umewekwa kwa muda.

Kulingana na Recep Tayyip Erdogan, Taliban wanata kulinda usalama wao wenyewe, wakati Uturuki - hususan kampuni za Uturuki, zingeweza kushughulikia vifaa vya miundombinu. Pendekezo hilo linaibua swali la usalama wa raia wa Uturuki ambao watafanya kazi katika uwanja wa ndege wa Kabul bila askari wa Uturuki, baada ya uwanja huu wa ndege kushambuliwa Alhamisi wiki hii katika shambulio ka kujitoa muhanga na rais Erdogan mwenyewe ana wasiwasi juu ya "ombwe kubwa la utawala" nchini Afghanistan kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.