Pata taarifa kuu
UFILIPINO-SIASA

Ufilipino: Rais Rodrigo Duterte atangaza kuachana na siasa na kutowania katika uchaguzi wa urais

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametangaza Jumamosi hii kwamba hatawania kwenye nafasi ya makamu wa rais mnamo mwaka 2022 na ataachana na siasa, akimuandalia njia binti yake kumrithi kama rais wa taifa hilo.

Jumamosi hii, Oktoba 2, Rodrigo Duterte ametangaza kwamba hatogombea kwenye nafasi ya makamu wa rais mnamo mwaka 2022 na atastaafu katika siasa.
Jumamosi hii, Oktoba 2, Rodrigo Duterte ametangaza kwamba hatogombea kwenye nafasi ya makamu wa rais mnamo mwaka 2022 na atastaafu katika siasa. REUTERS/Romeo Ranoco
Matangazo ya kibiashara

"Wafilipino wengi wanaungana na msimamo huo, na ni kwamba itakuwa ukiukaji wa Katiba" kuwania kwenye nafasi ya makamu wa rais, amesema Rodrigo Duterte. "Leo, ninatangaza kuachana na siasa na sintowania katika uchaguzi mnamo mwaka 2022," ameongeza.

Rodrigo Duterte, ambaye kura ya maoni inaonyesha kuwa bado ni maarufu kama vile aliposhinda uchaguzi wa urais mnamo mwaka 2016 kwa kuahidi kumaliza tatizo la dawa za kulevya, pamoja na mambo mengine, hairuhusiwi kikatiba kuwania muhula wa pili.

Mwishoni mwa mwezi  wa Agosti, alitangaza kuwania nafasi ya makamu wa rais wa nchi hiyo, akikusudia kuendelea na "vita vyake" dhidi ya dawa za kulevya na waasi. Habari hii ilishutumiwa mara moja na upinzani ambao waliona kama ana hofu ya kufunguliwa mashitaka.

Jumamosi hii, Oktoba 2, Rodrigo Duterte ametoa taarifa hii isiyotarajiwa mahali mahali ambapo alitarajiwa kujiandikisha kugombea kwenye nafasi ya makamu wa rais. Hakuweka bayana ni lini ataachana na kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.