UFILIPINO-USHIRIKIANO
Ufilipino: Duterte arejesha makubaliano kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Marekani
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejesha makubaliano ya kuhusiana na uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Ufilipino, mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili wametangaza Ijumaa.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Makubaliano hayo, yanayoitwa "Visiting forces agreement" (VFA), yanahusiana na uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Marekani ambao huja Ufilipino kushiriki mazoezi ya kijeshi.
Mkataba huu umechukua umuhimu zaidi wakati Marekani na washirika wake watalazimika kukabiliana na China inayozidi kujiimarisha kijeshi.
Mwaka jana Rodrigo Duterte alitangaza kufutwa kwa VFA, lakini hatimaye ameisasisha hadi mwezi Desemba