Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Macron na Modi waahidi "kushirikiana" katika ukanda wa Indo-Pacific

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wamezungumza Jumanne katikati ya mgogoro wa manowari za Australia na kusisitiza dhamira yao "ya kufanya kazi kwa pamoja kwa uwazi katika ukanda wa Indo-Pacific", Ikulu ya Elysée.

Emmanuel Macron akisalimiana na Narendra Modi katika Ikulu ya Elysée.
Emmanuel Macron akisalimiana na Narendra Modi katika Ikulu ya Elysée. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa "ametoa wito kujitolea kwa Ufaransa kuchangia kuimarisha uhuru wa kimkakati wa India, ikiwa ni pamoja na ngome zake za kiviwanda na teknolojia kama sehemu ya uhusiano wa karibu uliojengeka kwa misingi ya kuaminiana na kuheshimiana", imongeza ofisi ya Emmanuel Macron.

Viongozi hao wamesema watashirikiana katika eneo hilo ikiwa ni siku chache baada ya Australia kujiondowa kwenye mkataba wa kibiashara wa nyambizi na Ufaransa na badala yake ikaingia kwenye makubaliano na Marekani ya kupata nyambizi kama sehemu ya muungano mpya wa kijeshi pamoja na Marekani na Uingereza.

Ufaransa imeghadhabshwa na hatua ya Marekani ya kuongoza kwa siri mazungumzo kuhusu muungano mpya wa kimkakati wa kijeshi unaofahamika kama AUKUS pamoja na makubaliano ya kuiuzia Australia nyambizi za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.