Pata taarifa kuu
CANADA-CHINA

Canada: Hakuna uamuzi katika kesi ya Michael Spavor

Kesi ya Michael Spavor, mmoja kati ya raia wawili wa Canada wanaoshikiliwa nchini China tangu mwaka 2018 na kushtakiwa kwa ujasusi, imesikilizwa leo Ijumaa lakini mahakama haikutoa uamuzi, kulingana na mwanadiplomasia mmoja wa Canada.

China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi  Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani.
China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani. AP
Matangazo ya kibiashara

Michael Spavor ameonekana kwenye kesi hiyo, amesema Jim Nickel, mwanadiplomasia wa Canada katika ubalozi wa nchi hiyo nchini China.

China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi  Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani.

Beijing inasisitiza kuwa kukamatwa kwa raia hao wawili wa Canada hakuhusiani na kukamatwa kwa Meng Wanzhou, ambaye bado yuko chini ya kifubgo cha nyumbani huko Vancouver wakati akipambana dhidi ya kutumwa kwake Marekani.

Mazungumzo kati ya Marekani na China

Kwa mujibu wa Guy Saint-Jacques, balozi wa zamani wa Canada huko Beijing, kufunguliwa kwa kesi hiyo kunaambatana na mkutano kati ya Marekani na China, ambao unataka kuweka shinikizo kwa utawala wa Biden kupata Meng Wanzhou aachiliwe huru.

Kesi ya Michael Kovrig, mwanadiplomasia wa zamani, inatarajiwa kufunguliwa Jumatatu wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.