Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Maelfu ya watu wahamishwa kufuatia mafuriko Wales

Watu zaidi ya Elfu 18 nchini Australia wamehamishwa katika maeneo salama Kusini mwa Wales, kufuatia mafuriko makubwa yanayosababisha na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Mashariki mwa Pwani ya nchi hiyo.

Nyumba kadhaa zimesombwa na maji katika maeneo mbalimbali ya Australia kutokana na mafuriko,
Nyumba kadhaa zimesombwa na maji katika maeneo mbalimbali ya Australia kutokana na mafuriko, AP - Mark Baker
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha mito na mabwawa kujaa karibu na jiji kuu Sydney, wakati huu watalaam wa hali ya hewa wakionya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi.

Waziri Mkuu Scott Morrison amesema serikali imepanga kutoa fedha kuwasaidia wale wote waliolazimika kuondoka makwao kutokana na janga hili ambalo limeelezwa hutokea mara mojha, kila baad aya miaka hamsini katika jiji la Sydney.

 Mpaka sasa, kuna madhara makubwa yanayoendelea kushuhudia katika jiji la Sydeny ambako kunahsuhudiwa kujaa lkwa maji ikiwemo barabara, magari na mlaakzi ya watu.

 Watu zaidi ya Milioni 25 wanatarajiwa kuathrika na mafuriko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.