Pata taarifa kuu
CHINA

Kesi ya Michael Kovrig yaanza kusikilizwa China

Kesi dhidi ya Mwanadiplomasia Michael Kovrig,raia wa Canada anayezuiwa nchini China kwa zaidi ya miaka miwili sasa kwa madai ya kuwa jasusi wa kigeni nchini humo, imeanza jijini Beijing.

China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi  Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani
China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani Fred DUFOUR POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuzuiwa kwa Kovrig, kumesababisha uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya China na Canada baada ya raia mwingine wa Canada Michael Spavor kushtakiwa kwa makosa kama hayo kufuatia Canada kumzuia raia wa China Meng Wanzhou  Mkurugenzi wa kampuni ya Huawei anayetakiwa na Marekani .

China ilimkamata Michael Spavor na Michael Kovrig baada ya kukamatwa kwa afisa mkuu wa kifedha wa kampuni ya simu ya China ya Huawei, Meng Wanzhou, mwezi  Desemba 2018 huko Vancouver. Meng Wanzhou alitakiwa kusafirishwa nchini Marekani.

Beijing inasisitiza kuwa kukamatwa kwa raia hao wawili wa Canada hakuhusiani na kukamatwa kwa Meng Wanzhou, ambaye bado yuko chini ya kifubgo cha nyumbani huko Vancouver wakati akipambana dhidi ya kutumwa kwake Marekani.

Jim Nickel Balozi wa Canada nchini China amesema juhudi za kumwona Kovrig zimegonga mwamba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.