Pata taarifa kuu
JAPAN-SUGA-SIASA-USALAMA

Yoshihide Suga kuapishwa kama Waziri Mkuu wa Japan

Yoshihide Suga, 71, kiongozi mpya wa chama cha Liberal Democratic Party (PLD), chama tawala nchini Japan, anatarajiwa kuapishwa kuwa Waziri Mkuu leo Jumatano, kuchukua nafasi ya Shinzo Abe ambaye alijiuzulu kwa sababu za kiafya.

Yoshihide Suga, Waziri Mkuu mteule wa Japan, Tokyo, Septemba 16, 2020.
Yoshihide Suga, Waziri Mkuu mteule wa Japan, Tokyo, Septemba 16, 2020. CHARLY TRIBALLEAU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Saa arobaini na nane baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa ndani katika chama cha PLD, kumtafuta atakaye chukuwa mikoba ya Shinzo Abe, Yoshihide Suga amepitishwa na Baraza la Wawakilishi pamoja na Bunge la Seneti kabla ya kuapishwa kama waziri mkuu mpya wa Japan.

Zoezi la kupiga kura limefanyika mapema alasiri saa za Japan, baada ya kujiuzulu kwa pamoja serikali ya Abe mapema leo asubuhi.

Bw. Suga amekuwa katibu na msemaji wa serikali tangu Shinzo Abe aliporudi madarakani mwishoni mwa mwaka 2012.

Yoshihide Suga ambaye ni kutoka familia ya wakulima alizaliwa Desemba 6, 1949.

Aliwakilisha jimbo la uchaguzi Kanagawa 2 katika Baraza la Wawakilishi la Japani tangu mwaka 1996. Alifanya kazi kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Mawasiliano wakati wa awamu ya kwanza ya Shinzo Abe kama Waziri Mkuu kutoka 2006 hadi 2007, na kama Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wakati wa awamu ya pili ya Abe kutoka 2012 hadi 2020.

Muda wake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ulikuwa mrefu zaidi katika historia ya Japani. Suga alitangaza kugombea kwake katika uchaguzi wa uongozi wa LDP mwaka 2020 kufuatia tangazo la Abe la kujiuzulu, na alizingatiwa sana kuwa kiongozi wa kumrithi Abe kama waziri mkuu, baada ya kupata idhini kutoka kwa washiriki wengi wa kura katika chama kabla ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.