Pata taarifa kuu
JAPAN-ABE-SIASA-USALAMA

Mrithi wa Shinzo Abe kujulikana Septemba 14

Chama tawala nchini Japan cha Liberal Democratic Party (PLD) kimethibitisha leo Jumatano kwamba zoezi la kumteua mrithi wa Shinzo Abe, waziri mkuu ambaye amejiuzulu kwa sababu za kiafya, litafanyika Septemba 14.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu  mwaka 2007.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu mwaka 2007. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Mshirika wa karibu wa Bw. Abe, Yoshihide Suga, ndiye anaanayepewa nafasi kubwa kuchukuwa wadhifa huo.

Uchaguzi huu wa ndani, ambao kampeni yake rasmi itaanza Septemba 8, utafuatiwa na zoezi la upigaji kura katika Bunge, Septemba 16.

Lakini hatua hii ya mwisho ya kumchagua Waziri Mkuu itakuwa tu ya kawaida, kwani chama cha PLD na mshirika wake chama cha Komeito, kinadhibiti wingi wa viti katika taasisi mbili za bunge.

Yoshihide Suga, katibu mkuu Kiongozi wa sasa wa serikali mwenye umri wa miaka 71, anatarajia kutangaza rasmi nia yake ya kuwania kwenye nafasi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari baadaye Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.