Pata taarifa kuu
JAPANI-SIASA-USALAMA

Japani: Chama cha PLD kukutana kuhusu uteuzi wa mrithi wa Shinzo Abe

Kamati kuu ya chama tawala cha Liberal Democratic Party (PLD) nchini Japani, kwa kauli moja imeamua kwamba kiongozi mtarajiwa wa chama hicho, ambaye kuna uwezekano wa kuwa waziri mkuu, atachaguliwa kwa kura katika muundo uliorahisishwa ili kuokoa muda, mwakilishi mwandamizi wa PLD amesema.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu  mwaka 2007.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu mwaka 2007. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Mbio za kumrithi Shinzo Abe katika muundo kamili zingehitaji miezi miwili ya maandalizi na kutakuwa na athari kwenye bajeti na kwa maamuzi yanayohusiana na mgogoro wa afya unaosababishwa na virusi vya Corona, mwenyekiti wa Kamati kuu ya PLD, Shunichi Suzuki, amesema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa baraza hilo.

Siku ya Ijumaa Shinzo Abe alitangaza kuwa anaachia ngazi, akitoa sababu za kiafya.

Chama cha PLD kinatarajia kumteua mrithi wa Abe kwenye uongozi wa chama Septemba 14, na mshindi atateuliwa kuwa waziri mkuu kwa sababu ya idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha PLD.

Kulingana na taarifa kutoka televisheni ya serikali ya NHK, kundi moja kuu la wafuasi wa chama cha PLD linaunga mkono Katibu Mkuu Kiongozi wa sasa wa serikali, Yoshihide Suga, mshirika wa karibu wa muda mrefu wa Shinzo Abe, kwania kwenye nafasi hiyo.

Suga hajatangaza hadharani nia yake ya kuwania kwenye nafasi hiyo ya kumrithi Shinzo Abe, lakini amemuelezea mtu moja kuwa yuko tayari kuwania kwenye uongozi wa chama, chanzo hicho kimeliambia shirika la habari la REUTERS.

Vyombo vya habari kadhaa vya nchini Japan vimeripoti kwamba Suga alikuwa amepanga kurasimisha nia yake ya kuwania kwenye uongozi wa chama Jumatano wiki hii na kutangaza nia yake ya kuendelea na sera iliyoanzishwa na Shinzo Abe, haswa katika nyanja ya uchumi.

Waziri wa zamani wa Ulinzi Shigeru Ishiba na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Fumio Kishida wametangaza nia yao ya kukuwania kwenye nafasi hiyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa sasa, Toshimitsu Motegi, amesema leo Jumanne kwamba bado hajachukuwa uamuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.