Pata taarifa kuu
JAPAN-ABE-SIASA-USALAMA

Japan: Waziri Mkuu Shinzo Abe kujiuzulu kwa sababu za kiafya

Waziri Mkuu Shinzo Abe, 65, anapanga kutangaza Ijumaa hii, Agosti 28, nia yake ya kujiuzulu kwa sababu ya matatizo ya kiafya, kulingana na vyombo kadhaa vya habari nchini Japani, bila hata hivyo kutaja chanzo.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu  mwaka 2007.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi kujiuzulu mwaka 2007. KIM KYUNG-HOON / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na kituo cha televisheni ya serikali ya NHK, waziri mkuu, ambaye amepatwa na ugonjwa wake wa zamani wa matumbo sugu, ameelezea "nia yake ya kujiuzulu ili kuepuka kuvuruga hali ya kisiasa ya kitaifa".

Bwana Abe anashikilia wadhifa wake bila kukatizwa tangu mwishoni mwa mwaka 2012, rekodi ya kipindi kirefu kwa waziri mkuu wa Japani.

Ifahamu Japan, nchi yenye safu ya milima

Japani ni nchi ya visiwa katika Pasifiki, mkabala wa mwambao wa mashariki ya Asia. Wajapani wenyewe hutumia jina la "Nihon" au "Nippon" lenye maana ya "Mwanzo wa jua". Hivyo Japani huitwa pia "Nchi ya Macheo".

Nchi ina eneo la km² 377.944; na wakazi milioni 127; idadi hiyo imeanza kupungua.

Japani ni kati ya nchi za dunia zilizoendelea sana upande wa sayansi, teknolojia na uchumi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda.

Japani ni funguvisiwa lenye visiwa zaidi ya 3.000 mbele ya pwani ya Uchina, Korea na Urusi (Siberia).

Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano mkubwa wa wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka sakafu ya bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo.

Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete la moto la Pasifiki linalozunguka bamba la Pasifiki.

Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.