Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND-MAUAJI-USALAMA-HAKI

Mauaji ya Christchurch huko New Zealand: Brenton Tarrant ahukumiwa kifungo cha maisha

Kesi ya kigaidi ya Brenton Tarrant, mhusika wa mashambulio dhidi ya msikiti wa Christchurch, mwezi Machi 2019, imemalizika leo Alhamisi, Agosti 27 baada ya kusikilizwa kwa muda wa siku tatu.

Tangu mwezi Machi mwaka huu Tarrant alikubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. Mshambuliaji huyo alisema anakiri kuwa na hatia ya kuwauwa waumini 51, na jaribio la kuwauwa wengine 40 katika mashambulizi ya bunduki aliyoyafanya mwezi Machi mwaka 2019.
Tangu mwezi Machi mwaka huu Tarrant alikubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. Mshambuliaji huyo alisema anakiri kuwa na hatia ya kuwauwa waumini 51, na jaribio la kuwauwa wengine 40 katika mashambulizi ya bunduki aliyoyafanya mwezi Machi mwaka 2019. John Kirk-Anderson/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Brenton Tarrant hana tena nafasi ya kukata rufaa na amehukumiwa kifungo cha maisha, wakati hakuna uwezekano wa kuachiliwa kwa dhamana.

"Muuaji mbaya kabisa katika historia ya New Zealand," mwendesha mashtaka wa Mahakama Kuu ya Christchurch Mark Zarifeh alimwita Brenton Tarrant, mhusika wa mashambulio ya misikiti ya Christchurch.

Raia kutoka Australia mwenye umri wa miaka 29, aliyepatikana na hatia ya mauaji ya watu 51, wote kutoka jamii ya Waislamu, mwezi Machi 15, 2019, amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila kuepo na uwezekano wa kuachiliwa kwa dhamana.

Hukumu hiyo kuhusu kitendo cha kigaidi ni ya kwanza katika historia ya New Zealand. Wakati wa uamuzi huo, Jaji Cameron Mander amemwambia mtuhumiwa: "Haujaonyesha huruma, wala haujaomba msamaha ... hakuna shaka kuwa ulikuja New Zealand kwa lengo tu la kuangamiza jamii ya Waislamu".

Jaji amehitimisha kwa maneno haya: "Kitendo hicho hakuna anayeweza kukifumbia macho nchini hapa... hata popote pale duniani."

"Natumai hii ni mara ya mwisho kuwa na sababu ya kusikia au kusema jina la gaidi hapa nchini. Anastahili kunyamanzishwa kabisa, "Waziri Mkuu Jacinta Ardern amesema.

Katika mashambulizi ya Machi 2019, Tarrant aliwashambulia kwa bunduki za rashasha waumini waliokuwa kwenye ibada katika msikiti wa Al Noor na Linwoood mjini Christchurch.

Tangu mwezi Machi mwaka huu Tarrant alikubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. Mshambuliaji huyo alisema anakiri kuwa na hatia ya kuwauwa waumini 51, na jaribio la kuwauwa wengine 40 katika mashambulizi ya bunduki aliyoyafanya mwezi Machi mwaka 2019.

Pia alikiri kuwa na hatia kwa kuhusika katika tendo la kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.