Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-HONG KONG-USALAMA-SIASA

Hong Kong: Trump asaini sheria inayowawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa China

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini sheria inayoagiza nchi hiyo kulitambua eneo la Hong Kong kama la upendeleo, hatua inayokuja baada ya China kupitisha sheria mpya za usalama kuhusu eneo hilo.

Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Juni 26, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House, Juni 26, 2020. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Trump amesema kuwa Hong Kong sasa itatambuliwa kama China, huku akiongeza kuwa ametia saini maazimio ya bunge yanayowawekea vikwazo raia wa China wanaodaiwa kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Hong Kong.

"Sheria hii inaupa utawala wangu zana mpya zenye nguvu kuwawajibisha watu na taasisi ambazo zimehusika kuipokonya Hong Kong uhuru wake. Sote tumeona kile kilichofanyika. Si hali nzuri. Uhuru wao umechukuliwa, haki zao zimechukuliwa, na kwa maoni yangu kutokana na hayo Hong Kong haipo kwa sababu, haitaweza tena kushindana na masoko huru.” Amesema Trump.

Hatua hii ya Marekani imeikasirisha China ambayo imesema italipiza kisasi dhidi ya hatua hiyo ya Trump, itakayoruhusu pia mabenki kuwekewa vikwazo kuhusiana na hatua yake dhidi ya Hong Kong.

“China itatoa majibu yanayostahiki ili kuyalinda masilahi ambayo ni halali, na pia itaweka vikwazo kwa maafisa wa Marekani na kampuni zake, “ wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema katika taarifa.

Uhusiano kati ya Marekani na China umekuwa mbaya zaidi, tangu mataifa hayo mawili yaliposaini awamu ya kwanza ya makubaliano ya biashara lakini hadi sasa mazungumzo hayo yamekwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.