Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-PELL-HAKI

Australia: Kardinali Pell, aliyehukumiwa mwaka 2018 kwa unyanyasaji wa kijinsia, aachiliwa huru

Kardinali wa zamani George Pell ameachiliwa huru baada ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya Australia. Mwezi Desemba 2018 alihukumiwa hadi miaka sita jela kwa unyanyasaji wa kijnsia dhidi ya watoto wawili katika miaka ya 1990, wakati alikuwa Askofu Mkuu wa Melbourne.

Kardinali George Pell aachiliwa huru Jumanne hii, Aprili 7, 2020.
Kardinali George Pell aachiliwa huru Jumanne hii, Aprili 7, 2020. William WEST / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutumikia kifungo chake kwa zaidi ya mwaka mmoja katika jela la Melbourne, muweka hazina wa zamani wa Vatikani George Pell ameachiliwa leo Jumanne Aprili 7.Uamuzi huo umewashangaza wengi nchini Australia.

Mahakama Kuu ya Australia imebaini kwamba majaji waliomhukumu kwa magai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto mnamo mwezi Desemba 2018, hawakutilia manani ushahidi uliyotolewa na upande wa utetezi.

Mahakama Kuu inasema ushahidi uliyotolewa na mmoja wa waathiriwa ulikuwa wa kuaminika na wa kweli, lakini ushahidi huo haukuwa unatosha na ndio sababu George Pell almeachiliwa huru.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umeleta gumzo kubwa nchini Australia, huku George Pell ambaye amewahi kudai kuwa hana hatia, akikaribisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.