Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Australia yafunga mipaka yake kwa raia wa kigeni

Australia imechukua nyayo za mataifa mengine duniani kufunga mipaka yake kwa raia, ambao si wakaazi au wenyeji wa taifa hilo wanaoingia nchini humo katika kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Covid-19.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema nchi yake itaanzisha marufuku ya kusafiri Ijumaa wiki hii kwa watu ambao si raia wa Australia au hawaishi nchini humo ili kupunguza kuenea kwa virusi vya ugonjwa Covid-19.
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema nchi yake itaanzisha marufuku ya kusafiri Ijumaa wiki hii kwa watu ambao si raia wa Australia au hawaishi nchini humo ili kupunguza kuenea kwa virusi vya ugonjwa Covid-19. AAP Image/James Ross/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema nchi yake itaanzisha marufuku ya kusafiri Ijumaa wiki hii (saa 10:00 asubuhi saa za kimataifa) kwa watu ambao si raia wa Australia au hawaishi nchini humo ili kupunguza kuenea kwa virusi vya ugonjwa Covid-19.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kupitia televisheni huko Canberra, Scott Morrison ametetea uamuzi huo kwa kusema kwamba idadi kubwa ya kesi za maambukizi ziliingia nchini Australia kutoka nchi za kigeni.

Nchini Australia sasa hivi kunaripotiwa kesi 600 za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 na vifo sita vilivyotokana na ugonjwa huo, ikiwa ni idadi ndogo ikilinganishwa na nchi zingine ambazo tayari zimeathiriwa na ugonjwa huo, lakini mamlaka ina wasiwasi ya kuongezeka visa vingi vipya vya maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.