Pata taarifa kuu
INDIA-UCHUMI-USALAMA

India: Maelfu walazwa hospitali kufuatia kuvuja kwa gesi katika moja ya kiwanda Vishakapatnam

Tukio la kuvuja kwa gesi limetokea katika kiwanda cha kutengeneza vifaa vya plastiki Alhamisi, Mei 7 huko Vishakapatnam, mji mkuu wa jimbo la Andhra Pradesh, Kusini mwa India.

Zoezi la uokoaji likiendelea huko Vishakhapatnam baada ya kuvuja kwa gesi mbaya katika kiwanda cha LG Polymers Mei 7, 2020.
Zoezi la uokoaji likiendelea huko Vishakhapatnam baada ya kuvuja kwa gesi mbaya katika kiwanda cha LG Polymers Mei 7, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu 6 wamefariki dunia na maelfu wengine wamelazwa hospitalini. Zaidi ya watu 3,000 wanahamishwa ili kuepuka hasara zaidi kutokea.

Tukio hilo limetokea karibu saa tisa usiku katika kampuni ya kutengeneza bidhaa za plastiki ya LG Polymers kutoka Korea Kusini. Kiwanda hicho kinapatikana karibu na eneo la makazi la Vishwanapatnam, mji mkuu wa jimbo la kusini la Andhra Pradesh.

Kiwanda hiki kilikuwa kimefungwa kwa mwezi mmoja sasa baada ya serikali kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona. Kiwanda hicho kimekuwa kikizindua shughuli za uzalishaji wakati kioevu cha sumu kilipovuja na kugeuka kuwa gesi, mwandishi wetu nchini India, Sébastien Farcis, ameripoti.

India iko katika hali ya tahadhari tangu mwishoni mwa mwezi Machi kama sehemu ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, huku uchumi wake ukiendelea kukwama wakati shughuli nyingi zimesimama kabisa.

Waziri wa Viwanda katika Jimbo la Andhra Pradesh amehakikisha kwamba tukio hilo la uvujaji limedhibitiwa haraka, lakini athari tayari ni mbaya kwa maelfu ya watu wanaoishi karibu na kiwanda hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.