Pata taarifa kuu
INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: India yatangaza kesi zaidi ya 10,000, hatua ya tahadhari kuendelea hadi Mei 3

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameagiza kuongezwa kwa muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maamukizi ya virusi vya Corona hadi Mei 3.

Waziri Mkuu wa India amesema kila Mhindi ataendelea kubaki nyumbani hadi Mei 3.
Waziri Mkuu wa India amesema kila Mhindi ataendelea kubaki nyumbani hadi Mei 3. REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

Ni wiki ya tatu sasa tangu serikali ya India kuchukuwa hatua ya kuwataka raia kubaki nyumbani katika kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, wakati idadi ya visa vya maambukizi imevuka watu 10,000 katika nchi hii yenye watu bilioni 1.3."

"Kila Mhindi ataendelea kubaki nyumbani hadi Mei 3. Natoa wito kwa Wahindi wote waache kueneza ugonjwa huo kwa maeneo mapya," amesema Narendra Modi katika hotuba kwenye televisheni.

Kulingana na data iliyotolewa Jumanne na serikali ya India, idadi ya visa vya maambukizi kutokana na Corona sasa imefikia watu 10,363, pamoja na vifo 339.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.