Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Mlipuko wa virusi vya Corona wazua wasiwasi mkubwa China na kote duniani

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi hatari vya Corona imeongezeka zaidi Jumatano nchini China, ambapo mamlaka inasema watu tisa wamefariki dunia.

Kituo cha treni  cha Hankou huko Wuhan, mkoa wa kati wa China wa Hubei, Januari 21, 2020.
Kituo cha treni cha Hankou huko Wuhan, mkoa wa kati wa China wa Hubei, Januari 21, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini China imeonya kwamba virusi hivyo hatari vinaweza "kusambaa" kwa urahisi zaidi.

Taarifa zaidi zinasema idadi ya walioathiriwa na virusi hivyo imefikia karibu watu 300.

Wakati huo huo nchi nyingi za bara la Asia zimeimarisha udhibiti zaidi kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo vinavyofanana na virusi vya SARS, vilivyosambaa kutoka China kwa nchi kadhaa mwaka 2002-2003.

Baadhi ya mataifa yameanza kuchukua hatua za tahadhari kwa kuwapima wasafiri wanaotoka China hasa Wuhan.

Hofu ya kusambaa kwa virusi vya Corona imetanda zaidi baada ya mtaalamu wa serikali ya China Zhong Nanshan kuweka wazi kupitia televisheni ya Taifa kuwa virusi hivyo vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Mji wa Wuhan ndio unaoripotiwa kuwa na visa vingi zaidi vya ugonjwa huo kwa kuwa na wagonjwa 258. Mjini Beijing, zaidi ya watu 20 wameripotiwa kupata maambukizi. Miji mingine iliyoarifiwa kuwa na visa vya virusi hivyo ni pamoja na Shanghai na kusini mwa jimbo la Guangdong. Korea Kusini, Japan na Thailand ambako kuna wasafiri wengi kutoka China kumeripotiwa visa vinne vya ugonjwa huo.

Jana Jumanne Mamlaka nchini China zilithibitisha kwamba virusi hivyo huenda vikasambazwa kupitia maingiliano ya binadamu ambapo inaripoti kwamba wafanyakazi 15 wa huduma za matibabu wameambukizwa na mmoja amefariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.