Pata taarifa kuu
CHINA-AFYA

Corona: Maambukizi kupitia maingiliano ya binadamu yathibitishwa, sita wafariki dunia China

Mtu wa sita ameripoitwa kufariki dunia kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi hatari vya Corona huko Wuhan, mji ulio katikati mwa China. Tume ya kitaifa ya afya siku ya Jumatatu ilithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo yanaweza kusambaa kupitia wanadamu.

Ugonjwa huo mara ya kwanza uligunduliwa mjini Wuhan, mji uliopo katikati ya China ulio na idadi ya watu milioni 11 , mwaka uliopita. Kuna takriban visa 218 vya virusi nchini China kwa mujibu wa WHO.
Ugonjwa huo mara ya kwanza uligunduliwa mjini Wuhan, mji uliopo katikati ya China ulio na idadi ya watu milioni 11 , mwaka uliopita. Kuna takriban visa 218 vya virusi nchini China kwa mujibu wa WHO. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

China imethibitisha kesi 291 za maambukizi kufikia Januari 20. Mlipuko wa virusi vya Corona ambavyo vilianzia kwenye mji wa Wuhan katikati mwa China umesababisha mtikisiko kwenye masoko ya fedha wakati shirika la afya duniani WHO likiitisha mkutano hapo Jumatano wiki hii kufikiria uwezekano wa kuutangaza mlipuko huo kuwa ni dharura ya kiafya ya kimataifa.

Virusi hivyo vipya ambavyo vina hatari ya kusambaa zaidi wakati wa kipindi cha mwaka mpya wa China kutokana na kuwa watu wengi husafiri, kwa mujibu wataalam wa afya.

Hata hivyo mamlaka nchini China wanasema wameanza kuchukuwa hatua kubwa za tahadhari ikijitahidi kudhibiti mripuko huo wa virusi hatari.

Mamlaka nchini China leo zimethibitisha kwamba virusi hivyo huenda vikasambazwa kupitia maingiliano ya binadamu ambapo inaripoti kwamba wafanyakazi 15 wa huduma za matibabu wameambukizwa na mmoja amefariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.