Pata taarifa kuu
HONG KONG-USALAMA

Hong Kong: Sekta ya uchukuzi yakumbwa na sintofahamu, Carrie Lam akosoa waandamanaji

Operesheni ya kuzuia njia ya reli ya treni umeme ya mwendokasi iliyozinduliwa na waandamanaji wa wanaotaka demokrasia na uhuru zaidi Hong Kong imezorotesha shughuli katika sekta ya uchukuzi katika jimbo hilo, leo Jumatatu, Agosti 5 asubuhi, wakati mgomo unatarajia kuzorotesha shughuli nyingi katika mji huo.

Waandamanaji wazuia njia ya reli ya treni umeme ya mwendokasi.
Waandamanaji wazuia njia ya reli ya treni umeme ya mwendokasi. REUTERS/Eloisa Lopez
Matangazo ya kibiashara

Baada ya maandamano mawili jana Jumapili jioni, husa katika wilaya maarufu ya biashara ya Causeway Bay, waandamanaji wameingia mitaani mapema asubuhi katika vituo mbalimbali vya treni umeme za mwendokasi na kuzuia treni kuondoka.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika mtaa maarufu kwa utalii. Siku ya Jumamosi, wilaya ya Tsim Sha Tsui ambayo hujaa watalii na wafanyabishara kutokana na maduka na hoteli zake za kifahari, ilikumbwa na machafuko wakati makundi madogo ya waandamanaji sugu walikabiliana na polisi.

Wakati huo huo kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam ameonya kuwa mji huo unaharibiwa kutokana na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa kwa mwezi wa pili sasa.

Bi.Lam amesema kinachoshuhudiwa kwa sasa ni hatari mno, wakati huu polisi wanapoendelea kukabiliana na waandamanaji.

“Kuendelea kushuhudia uharibifu huu kwa sababu ya kutafuta mambo fulani, yanayoletewa na kundi ambalo halina mpango, linaharibu mji huu na kusababisha utovu wa usalama, kinachoendelea ni kuendelea kuharibu mji huu tunaoupenda, mji ambao tumeshirikiana kuuja kwa bidii, tukipitia nyakati ngumu, “ Carrie Lam.

Waandamanaji Hong Kong wameendelea kupinga mpango wa serikali ya eneo hilo kupitisha sheria itakayowawezesha wakaazi wa mji huo kushtakiwa nchini China, kwa kile wanachosema unawalenga wapinzani wa serikali ya Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.