Pata taarifa kuu
HONG KONG-CHINA-SIASA-MAANDAMANO

Mwanaharakati maarufu Joshua Wong aachiliwa huru huko Hong Kong

Mwanaharakati maarufu katika eneo la Hong Kong, Joshua Wong ameachiliwa huru baada ya kufungwa jela kutokana na harakati zake za kupanga maandamano dhidi ya uongozi wa  eneo hilo mwaka 2014.

Joshua Wong mwanaharakati maarufu akiachiliwa huru Juni 17 2019
Joshua Wong mwanaharakati maarufu akiachiliwa huru Juni 17 2019 REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Wong mwenye umri wa miaka 22, ametaka kuendelea kwa maandamano dhidi ya kiongozi wa Hong Kong, Carrie Lam, ambaye sasa ameanza kupata shinikizo za kujiuzulu.

Mwanaharakati huyo ambaye ni mwanafunzi alipata, umaarufu kubwa baada ya kuongoza maandamano makubwa mwaka 2014 kushinikiza uongozi wa Hong Kong kukubaliwa wakaazi kupewa nafasi ya kuwachagua viongozi wao.

Wakati huu, wakaazi wa Hong Kong wengi wakiwa vijana, wanaendeleza maandamano kukakataa mswada wa sheria ambao unapendekeza washukiwa wa makosa mbalimbali kufunguliwa mashtaka katika Mahakama za China.

Waandamanaji wanasema zaidi ya watu Milioni 2 walishiriki katika maandamano makubwa yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wakiendeleza kushinikiza uongozi wa Hong Kong kuachana kabisa na mswada huo ambao tayari umesitishwa.

Licha ya Bi. Lam ambaye anawakilisha serikali ya Beijing katika mji huo, kuomba radhi kwa utata kuhusu mswada huo, waandamanaji wameapa kuendelea kushinikiza kujiuzulu kwake.

Hata hivyo, serikali ya China imesema inasimama na kumuunga mkono Carrie Lam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.