Pata taarifa kuu
IRAN-ICJ-MAREKANI-VIKWAZO-UCHUMI

Iran yawasilisha malalamiko yake kwa ICJ dhidi ya vikwazo vya Marekani

Iran inatarajia kuomba Jumatatu wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuondoa vikwazo vya Marekani, ambavyo utawala wa Trump umetishia kuchukua.

Mji mkuu wa Iran, Tehran. (Picha ya kumbukumbu).
Mji mkuu wa Iran, Tehran. (Picha ya kumbukumbu). RFI/Muriel Paradon
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kurejesha vikwazo vya Marekani baada kukemea makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa mnamo mwaka 2015 kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Iran inasema kuwa kurejeshwa kwa vikwazo vya Marekani, ambavyo vinalenga kudhoofisha zaidi uchumi wake, ni ukiukaji wa mkataba ambao haujulikani sana, uliotiliwa saini mnamo mwaka 1955 kati ya nchi hizo mbili, "Mkataba wa Urafiki, Biashara na haki za kibinafsi ".

Marekani haijajibu rasmi malalamiko hayo, lakini wanasheria wake, ambao watasikilizwa Jumanne wiki hii, kuna uwezekano wajibu kwamba Mahakama haina uwezo wa kushughulikia kesi hiyo, kwamba mkataba huo ni wa kizamani na kwamba, hata kama mkataba haungelikuwepo, vikwazo havingeliathiri chochote.

ICJ mpaka sasa inabaini kwamba mkataba wa 1955 bado ni halali, ingawa ulitiliwa saini miaka 24 kabla ya mapinduzi ya Kiislamu, ambayo yalibadilisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Kesi hiyo itasikilizwa kwa muda wa siku nne. Uamuzi wa ICJ utatolewa ndani ya mwezi mmoja.

Maamuzi ya ICJ, taasisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutatua migogoro ya kimataifa, yanahesimishwa, lakini mahakama haina uwezo wa kuyaweka katika vitendo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.