Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Trump na Rouhani wajibizana vikali

Vita vya maneo vimeibuka kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, huku kila momja akitoa vitisho dhidi ya mwengine.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Uhasama baina ya Marekani na Iran unaendelea, baada ya Donald Trump kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi.

Hata hivyo rais Trump ameionya Iran 'isiijaribu Marekani'.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter rais Trump ameandika "Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia, iwapo itaitishia Marekani.”

Wakati huo huo, akihutubia kundi la Wamarekani wa asili ya Iran jimbo la California, Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema utawala wa Iran "unafanana zaidi na mafia badala ya serikali".

Awali rais wa Iran Hassan Rouhani alisema vita na Iran vitakuwa "vita zaidi ya vita vingine vyote".

Rais Donald Trump alitangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa Iran mwezi Mei na kuuita mpango uliooza na kero kwa raia wote wa Marekani.

Rais Trump alisema wakati huo kwamba mpango huo 'unaifaidi tu na kuiongeza nguvu Iran.'

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.